November 26, 2015


Simba imeendelea na mazoezi chini ya Kocha Dylan Kerr na msaidizi wake, Iddi Salim. Mazoezi hayo yamefanyika kwenye Uwanja wa Karume Ilala jijini Dar es Salaam, leo.



Mazoezi ya Simba yamekuwa makali sana na ilikuwa mazoezi mechi kati ya timu kubwa dhidi ya vijana ya Simba, mechi ambayo iliishia kwa wakubwa kushinda kwa mabao 2-0.


Kati ya waliokuwa wakijifua, mmoja wapo alikuwa ni Mganda Brian Majegwa ambaye tayari ameonyesha nia ya kuichezea Simba na kuachana na Azam FC.
  
Mazoezi hayo yalikuwa na ushindani mkubwa huku kila upande ukionekana umepania kushinda hasa.




Simba iko katika maandalizi kujiweka sawa kwa ajili ya Ligi Kuu Bara iliyokuwa imesimama kwa muda.

 ANGALIA PICHAZEEEE.










0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic