November 26, 2015


Na Saleh Ally
Zanzibar Heroes imepoteza mechi zake zote mbili za michuano ya Chalenji.


Imeanza kwa kuchapwa bao 1-0 dhidi ya Burundi, mechi ya pili ikatandikwa tena kwa mabao 4-0 dhidi ya Uganda.

sasa inakutana na Kenya ikiwa ni mechi yake ya mwisho kama ya kujifurahisha vile.

Zanzibar Hereos, moja ya timu zilizokuwa hazitabiriki katika michuano ya Chalenji kwa maana ya ugumu. Imepoteza karibu kila mchezo.

Huenda linawezekana likaonekana ni kama jambo la kawaida tu, lakini kuna mengi sana ya kuangalia katika soka la Zanzibar.

Timu hiyo kuchapwa mabao matano katika mechi mbili, kupoteza mechi zote mbili bila ya kufunga hata bao moja, lazima tukubali kuna tatizo.

Zanzibar sasa si soka uwanjani, badala yake ni soka mdomoni kwa kuwa malumbano ndiyo yenye nafasi kubwa zaidi badala ya soka la utendaji.

Soka la utndaji, watu wangekuwa wakijadili matokeo na uchezaji bora. Lakini sasa kila mmoja anamshitaki mwingine mahakamani au anamlaumu mwingine kwa kukosea.

Viongozi wa Zanzibar wana tatizo, lazima wajue malumbano yao yanaufanya mchezo wa soka kuwa sawa na siasa na wanapaswa kulirekebisha jambo hilo.

Hakuwezi kuwa na maendeleo kama mfumo wa sasa wa soka Zanzibar ndiyo unaonekana ni chachu. Lakini kila mmoja akubali katika nafsi kwa kulumbana kipuuzi ni kuuangamiza mchezo wa soka.

Zanzibar ina vipaji rundo hata sihitaji kutoa mifano. Lakini vurugu, chuki na ubabaishaji wa viongozi wengi wa soka Zanzibar, kunazidi kuiangamiza kisoka.

Najua baada ya muda, viongozi haohao ndiyo watakaokuwa wakiinua mdomo kuanza kulaumu kwamba wamesahauliwa, au Zanzibar imesahauliwa. Lakini wao ndiyo wanaoipotezea muda sasa kwa kulumbana tena kwa ajili ya matumbo yao.


Acheni ujinga, acheni kuua soka ya Zanzibar na kama mmeshindwa ondokeni na muache Wazanzibar wengine wenye mapenzi ya dhati na maendeleo yas oka, wafanye kazi hiyo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic