November 27, 2015



Pamoja na kupigwa mechi mbili za michuano ya Kombe la Chalenji, Zanzibar Heroes imeibuka na kuitwanga Kenya kwa mabao 3-1.

Zanzibar imeshinda kwa mabao hayo katika mechi yake ya mwisho huku Mcha Hamis na Seleman Kassim ‘Selmbe’ akifunga mawili katika mechi iliyopigwa mjini Awasa, Ethiopia.

Zanzibar ilianza michuano hiyo kwa kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Burundi kabla ya kuchapwa mabao 4-0 dhidi ya Uganda.

Lakini katika mechi ya leo mambo yalikuwa tofauti na Zanzibar ilionyesha soka safi kabisa huku ikiwapa Kenya wakati mgumu.
Wakenya waliokuwa wakiamini wangesawazisha, mambo yalizidi kuwa magumu kwao huku Zanzibar ikiongeza bao moja baada ya jingine.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic