November 24, 2015

Kikosi cha Zanzibar Heroes kinachoongozwa na nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’ kimeng’olewa katika michuano ya Chalenji inayoendelea nchini Wethiopia.

Zanzibar Heroes imefungwa mabao 4-0 na Uganda na kuwa kipigo chake cha pili baada ya kuanza michuano hiyo kwa kufungwa bao 1-0 na Burundi.
Kwa kipigo hicho, maana yake Zanzibar Heroes haina nafasi ya kusonga mbele kutoka Kundi B.
Mechi ya mwisho watakutana na Kenya ambao walianza michuano hiyo kwa kuituliza Uganda kwa kuichapa mabao.

Katika mechi ya leo, Zanzibar walionekana hawana nguvu kabisa ya mipango na muda mwingi The Cranes walitawala mchezo.


The Cranes chini ya Sredojevic Milutin ‘Micho’ wangeweza kushinda zaidi ya mabao hayo kama wangekuwa makini katika umaliziaji.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic