December 1, 2015

MAJEGWA WAKATI AKIWA AZAM FC. HAPA ANAPAMBANA NA JUMA ABDUL WA YANGA.
Ligi Kuu Bara itaendelea Desemba 12 baada ya mapumziko ya kipindi cha zaidi ya wiki mbili.


Wanasimba wanajua kikosi chao kitarejea katika ligi hiyo kwa kucheza na Azam FC na uongozi wa klabu hiyo umesema hauna masharti yoyote, kiungo Brian Majegwa kucheza dhidi yao.

Msemaji wa Azam FC, Jaffar Iddi ‘Mbunifu’ amesema baada ya klabu hiyo kumalizana na Simba, Majegwa raia wa Uganda ni mali ya Simba na wana uamuzi wa kila kitu.
 
MAJEGWA; SASA NI MALI YA SIMBA.
“Wao Simba ndiyo wataamua kama Majegwa acheze siku hiyo au la. Sisi kama Azam FC, tutakuwa hatuna masharti wala hatuna cha kuhoji.

“Wataamua kupitia benchi lao la ufundi wanachoona, sisi tutakwenda kupambana na Simba kwa ajili ya kupata pointi tatu, mengine yanabaki kwao,” alisema Jaffar.


Majegwa amtua Simba rasmi baada ya pande mbili kukutana na kumalizana ikiwa ni baada ya mzozo wa siku kadhaa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic