Klabu ya Ligi Kuu ya
Denmark inayomtaka kiungo nyota wa Azam FC, Farid Musa ni katika klabu
zinazosajili Waafrika wachache lakini wamekuwa na mafanikio.
Brondy IF iliyoanzishwa mwaka 1964 ni moja ya
timu bora nchini Denmark na kwa kipindi cha miaka 10 sasa imekuwa na mafanikio
kwa asilimia kubwa ingawa si asilimia ya juu sana.
MASHABIKI WA BRONDY WAKIIUNGA MKONO TIMU YAO. |
Wachezaji ambao
walitokea Afrika na kufanya vizuri sana katika kikosi hicho ni pamoja na Uche
Okwuchukwu aliyetokea Nigeria, Ousman Jallow (Gambia) na nahidha wa muda mrefu
wa Zambia, Chris Katongo.
Wachezaji wengi wa
kikosi hicho wamekuwa wakisajiliwa kutoka nchini Denmark.
Angalau nchi za jirani
za Norway, Sweden na Finland nazo zimekuwa na wachezaji wengi katika kikosi
hicho cha Brondy IF.
0 COMMENTS:
Post a Comment