December 2, 2015


Mshambuliaji wa Yanga, Donald Ngoma ameonyesha ni mtu makini asiyetaka mchezo na kazi yake.


Ngoma alionyesha hilo baada ya kuamua kubaki akifanya mazoezi binafsi baada ya yale ya pamoja kama timu kumalizika.

Ngoma alikuwa akipiga mikwaju ya penalti pekee yake mara tu baada ya Yanga kumaliza mazoezi kwenye Uwanja wa Boko Veterani jijini Dar es Salaam.

Mzimababwe huyo alisema alikuwa akifanya hivyo ili kujiweka vizuri katika kazi hiyo kwa kuwa amekuwa akikosa penalty mara kadhaa.


“Nataka kuhakikisha naifanya kazi ya kupiga penalty kwa uhakika, ndiyo maana nimeamua kufanya mazoezi,” alisema Ngoma ambaye tayari ameanza kuzivutia timu kubwa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic