December 1, 2015


Sergio Ramos ametangwa kuwa beki bora wa La Liga kwa msimu wa 2014-2015 katika sherehe za utoaji tuzo zilizofanyika jijini Barcelona usiku wa kuamkia leo.

Ramos amewapiga kumbo mabeki wawili nyota Piqué wa Barcelona na Otamendi aliyekuwa akikipiga Valencia lakini sasa yuko Man City ya England.
Baada ya kuchukua tuzo, Ramos aliwashukuru wachezaji wenzake na benchi la ufundi la Madrid kumuwezesha kubeba tuzo hiyo.
Naye kiungo kinda, James Rodrigues ambaye ndiyo msimu wake wa kwanza Madrid ameshinda tuzo ya kiungo bora wa La Liga kwa msimu wa 2014-2015.

James amewapiga kumbo wakongwe wa La Liga kama Antoine Griezmann wa Atletico Madrid na Andres Iniesta wa Barcelona.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic