February 13, 2016


Mbeya City imeionyesha Toto African namna ya kutembea katika jiji la Mbeya baada ya kuichapa kwa mabao 5-1 katika mechi ya Ligi Kuu Bara.

Ramadhani Chombo 'Redondo' aliifungia Mbeya City mabao mawili, vivyo hivyo Haruna Moshi 'Boban' naye akafunga mawili pia kabla ya Meshack Samwel kufunga la tano.

Mbeya City imeibuka na ushindi huo wa kishindo ikiwa inacheza kwa mara ya kwanza chini ya Kocha Mmalawi, Kinnah Phiri.


Mjini Tanga, African Sports wameamka baada ya kuichapa Mgambo Shooting kwa bao 1-0. Na Kagera Sugar ikagawana pointi na JKT Ruvu kwa sare ya bao 1-1.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic