February 13, 2016

OZIL-ARSENAL

Na Saleh Ally
MOJA ya matatizo makubwa yanayowabana wachezaji wa Tanzania na hata nchi jirani kwa kipindi hiki ni upigaji wa mikwaju ya penalti.

Inapotokea timu imepata penalti, utaona wachezaji wanagawanyika utafikiri dimbwi la maji limetupiwa jiwe, maji yote yanasambaa.

Wanaondoka eneo la tukio kwa kuwa kila mmoja, anaogopa lawama. Wanahofia kwa kuwa hakuna ambaye yuko tayari kupiga mkwaju wa penalti kwa kuwa hana uwezo wa kufunga.

Penalti ni ‘ugonjwa’ mkubwa kwa wachezaji wengi, huenda kila aliyekuwa akijiamini katika upigaji penalti katika timu kubwa za Yanga, Simba sasa hajiamini tena.

Yanga na Simba zina wastani mzuri zaidi wa kukosa penalti kuliko kufunga na inaonekana sasa unazidi kuwa ugonjwa mkubwa kwa kuwa jinamizi la kukosa, limechukua nafasi kubwa.

Kawaida utaona kama ni michuano na mmeingia katika upigianaji penalti baada ya sare wakati wa dakika za nyongeza. Katika penalti, anayekwenda kupiga wa kwanza ni yule anayeaminika.

MAHREZ-LEICESTER

Upigaji penalti kwa kiasi kikubwa unajumuisha suala la kisaikolojia. Anayepiga kwanza anapofunga huwajenga kisaikolojia wengine kwamba ni jambo linalowezekana. Hivyo kila mmoja anajiamini.

Kujiamini kunaongeza uwezo bora wa utendaji, yaani kila anayefuata atakuwa anajiamini na atapiga kupitia uwezo bora na sahihi alionao kupitia mazoezi.

Hapa utaona, hata kama unajiamini, pia una ujuzi. Basi muhimu kabisa ni mazoezi. Hili hufanyika mazoezini ili kupata watu sahihi katika upigaji penalti faulo za mifumo yote ya ‘direct kick’ na ‘indirect kick’.

Katika michezo, kipaji ni kitu bora na bahati kuu lakini mazoezi ni lazima ili kukiboresha na kukisaidia kipaji. Mazoezi humsaidia hata asiye na kupaji cha juu kucheza kwa uwezo wa juu kabisa.

Nimeanza na nyumbani kuhusiana na wachezaji wa nyumbani au wale wa nje wanaocheza soka hapa nyumbani namna ambavyo wamekuwa wakihofia upigaji penalti.

KOLAROV-MAN CITY

Nakukumbusha namna ambavyo upigaji mipira ya adhabu umekuwa ni wa kiwango cha chini kabisa. Huwezi kuwa na hofu kwa timu fulani kupata mpira wa adhabu nje ya 18, ukiamini utafungwa.

Lazima tukubali, bado makocha wengi na hata wachezaji wenyewe hawaoni suala hilo la upigaji penalti au mikwaju ya adhabu kama ni muhimu kwa kuongeza ubora wa kiwango, thamani ya mchezaji na nguvu ya kuisaidia timu kupata ushindi.

Nitakupa mfano mdogo tu, makocha wa England wamekuwa wakiwapanga wachezaji kwa vifungu kwa ajili ya adhabu hizo tatu wakiamini zina umuhimu sana katika uchezaji, utengenezaji ushindi na kuimarisha ubora au uimara wa kikosi katika ushambuliaji.

Wakati maandalizi ya kabla ya msimu, makocha wanakuwa wanalipa nafasi kubwa suala hilo. Wachezaji wanaanza kuonyesha kiwango chao cha upigaji penalti na aina zote za faulo.


Baada ya hapo, kocha anafanya mchujo na kubaki na majina matatu au manne kwa kila kitengo cha upigaji wa penalti, adhabu ya kuguswa au adhabu ya moja kwa moja.

Utaona mfano Arsenal, ukisema penalti ni Mikel Arteta, Santi Cazorla na Olivier Giroud. Ukisema faulo za moja kwa moja ni Cazorla, Giroud na Mesut Ozil. Kwa upande wa mipira ya faulo ya kugusa ni Alexis Sanchez, Cazorla, Ozil na Aaron Ramsey.

Unajua kwa nini haya yanafanyika? Kwanza ni kumjenga mchezaji kwamba ana jukumu. Kumtengenezea ushindani dhidi ya wenzake. Kila mmoja angependa kuwa mpigaji namba moja na si msaidizi au anayesubiri.

Pili, hili linamsaidia mchezaji wakati anaingia uwanjani anakuwa anajua kama itakuwa ni indirect kick au penalti, basi hilo ni jukumu. Tatu, mchezaji wakati anaingia uwanjani, kisakolojia anakuwa ameshajiandaa na lolote kuhusiana na jukumu analohusika.

Wachezaji wa Yanga na Simba au timu nyingine, wamekuwa wakianza kujiandaa mara tu baada ya mkwaju wa penalti kupatikana, jambo ambalo si sahihi.

Utaona katika timu nyingi, mfano Leicester City, Jamie Vardy si mpigaji penalti katika wale watatu, lakini kwa kuwa ana mabao mengi na wanataka kumpa hali ya kujiamini zaidi au kumsaidia kuwa mfungaji bora. Wanaweza kumpa mpira apige, lakini kabla ya hapo anakuwa ameandaliwa kwamba yeye ndiye atapewa mkwaju kama utatokea kulingana na hali halisi.

Penalti si bahati wala bahati nasibu, ni mazoezi, kujiamini na maandalizi ya kutosha na ya uhakika. Makocha lazima wawe na watu maalum ambao wanajiandaa kwa ajili ya jukumu hilo.


Utamaduni wa kupiga penalti kwa kuamini kipaji pekee, umepitwa na wakati. Wachezaji na makocha waliamini hilo na kulifanyia kazi. England na kwingineko kulikoendelea, uamuzi wa kutenga watu maalum, hauna maana wengine hawajui lakini wanajua mazingira ya upigaji penalti yanavyokuwa magumu kunapokuwa hakuna maandalizi sahihi.

LUKAKU-EVERTON


Yeyote anaweza kukosa, hata kama alijiandaa lakini waliofanya maandalizi wanaweza kukosa mara chache zaidi ukilinganisha na wale wanaoamini bahati na kipaji pekee.


HAWA NI WAPIGA PENALTI WA KLABU ZOTE ZA LIGI KUU ENGLAND 2015-16:
Club
Penalties
Direct Free kicks
Corners and Indirect Free Kicks
Arsenal
Arteta, Cazorla, Giroud
Sanchez, Cazorla, Özil
Sanchez, Cazorla, Özil, Ramsey
Aston Villa
Sinclair, Bacuna, Gestede
Sinclair, Bacuna, Gestede
Westwood, Grealish, N’Zogbia
Bournemouth
Wilson, Daniels, Murray
Ritchie, Arter, Gradel
Ritchie, Gradel, Arter
Chelsea
Hazard, Oscar, Fabregas
Oscar, Willian, Fabregas
Willian, Fabregas, Oscar, Pedro
Crystal Palace
Cabaye, Gayle, Jedinak
Cabaye, Puncheon, Jedinak
Puncheon, Cabaye, Sako
Everton
Lukaku, Barkley, Baines
MMirallas, Baines, Barkley
Mirallas, Baines, Barkley
Leicester City
Brady, Jelavic, Long
Mahrez, Drinkwater, Albrighton
Albrighton, Mahrez, James
Liverpool
Henderson, Benteke, Sturridge
Henderson, Milner, Coutinho
Henderson, Milner, Coutinho
Man City
Agüero, Toure, Kolarov
Toure, Kolarov, De Bruyne
De Bruyne, Silva, Nasri
Man United
Rooney, Mata, Herrera
Depay, Rooney, Mata
Depay, Rooney, Mata
Newcastle
Cisse, Riviere, Mitrovic
Colback, De Jong, Gouffran
Ayoze, Thauvin, Colback
Norwich
Hoolahan, Brady, Dorrans
Brady, Hoolahan, Redmond
Brady, Hoolahan, Redmond
Southampton
Tadic, Rodriquez, Ward-Prowse
Tadic, Ward-Prowse, Van Dijk
Ward- Prowse,  Tadic, Davis
Stoke City
Arnautovic, Adam, Bojan
Arnautovic, Adam, Shaqiri,
Adam, Shaqiri, Affelay
Sunderland
Gomez, Borini, Johnson
Larsson, M’Vila, Johnson
ALarsson, M’Vila, Johnson
Swansea
Gomis, Sigurdsson
Sigurdsson, Ki
Sigurdsson, Ki
Swansea City
Bony, Sigurdsson, Gomis
Sigurdsson, Shelvey
Sigurdsson, Ki
Tottenham Hotspur
Kane, Eriksen
Eriksen, Lamela, Kane
Kane, Townsend, Son
West Bromwich Albion
Berahino, Morrison, Gardner
Gardner, Brunt, Rondon
Brunt, Gardner, Morrison
West Ham United
Noble, Carroll
Payet, Zarate, Noble
Payet, Zarate, Lanzini

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic