February 9, 2016

SIMBA

Na Mohammed Soud, Shinyanga
Gumzo kubwa katika vitongoji vya mji wa Shinyanga ni kuhusiana na mechi ya Simba dhidi ya wenyeji wake Stand United.

Mechi hiyo itachezwa Jumamosi na tayari Simba wako mjini hapa huku vijiwe vingi gumzo likiwa ni mechi hiyo.

Simba ilicheza mechi ya kwanza kwenye Uwanja wa Kambarage mjini hapa na kuitwanga Kagera Sugar kwa bao 1-0.
Sasa ni zamu ya wenyeji ambao wanataka kujiweka sawa na kumuonyesha kazi mnyama Simba ambaye anaonekana kuamka na kushinda mechi tano mfululizo za Ligi Kuu Bara.
Lakini Stand wamekuwa wakijitapa, watakuwa wa kwanza kuisimamisha Simba ya kocha Jackson Mayanja raia wa Uganda.

Lakini Mayanja, amesema kikosi chake kinachotaka ni ushindi ili kuendeleza rekodi nzuri.

“Ushindi litakuwa jambo zuri, tunaamini kupumzika kutatusaidia tofauti na ilivyokuwa mechi dhidi ya Kagera, wachezaji walichoka baada ya kucheza mechi mfululizo,” alisema Mayanja.

STAND

Lakini Kocha Mfaransa, Patrick Liewig anaamini pamoja na ubora wa Simba, Stand United itawashangaza.


“Timu yangu in a vijana wengi zaidi. Tumefanya maandalizi mazuri, licha ya kuwa na majeruhi kadhaa, lakini tutawashangaza,” alisema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic