February 9, 2016

KERR


Kocha wa zamani wa Simba, Dylan Kerr ameonyesha bado ana machungu na kutupiwa kwake virago.

Wakati Simba inaendelea kuchanja mbuga, Kerr ameonekana bado ana machungu baada ya kuhoji kwa kwamba mbona Yanga haijamtimua Kocha Hans van der Pluijm.

“Ndiyo, mimi nilikuwa nimepoteza mechi mbili tu. Nikafukuzwa kazi, leo Pluijm kapoteza mechi moja na sare moja, sasa vipi hafukuzwi,” alisema Kerr.

Huenda Kerr amesahau kwamba Simba na Yanga ni timu tofauti, kila moja ina uongozi na maisha yake.
“Najua ni timu tofauti, lakini hizi zote ni timu kubwa. Ninachoeleza hapa ni kukuonyesha haki haikutendeka,” anaweka msisitizo.


Kerr alitimuliwa wakati Simba ikiwa Zanzibar ilipokuwa inashiriki michuano ya Mapinduzi. Mara baada ya kupigwa bao 1-0 na Mtibwa Sugar katika hatua ya nusu fainali, uongozi ukamuita jijini Dar es Salaam, ukampa haki zake na kumuaga. Kwa sasa melkuwa akielekeza macho yake nchini Afrika Kusini ambako inaelezwa huenda aka[ata timu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic