February 13, 2016

KIKOSI CHA CERCLE DE JOACHIM

Na Mwandishi Wetu, Curepipe
WAKATI Yanga ilitarajia kutua mjini hapa jana usiku, Watanzania wengi wangependa kuijua timu inayocheza nayo leo katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Cercle de Joachim ni mabingwa mara mbili mfululizo wa Mauritius. Yaani msimu wa 2013-14 na 2014-15.

Yanga itakuwa dimbani kwenye Uwanja wa Geoge V saa 9:30 Alasiri hapa, ambayo ni saa 10:30 nyumbani Tanzania.
Lakini, Kocha wao, Abdel ben Kacem anataka sasa wafanye vizuri katika michuano ya kimataifa, mara baada ya kushindwa kufanya hivyo msimu uliopita.

“Yanga ni timu kongwe ya Afrika tofauti na sisi, lakini tumejiandaa vizuri na matokeo bora tunataka yaanzie nyumbani,” alisema Kacem.

Wanajua haitakuwa rahisi, hofu ya Yanga bado ipo na kila mmoja anajua ni moja ya timu bora katika ukanda wa Kusini mwa Afrika na haijawahi kung’olewa katika michuano ya kimataifa na klabu zinazotokea visiwani, mfano Comoro au Mauritius.

Hata hivyo, ni timu iliyopata heshima ya kuwa na idadi lukuki ya mashabiki nchini mwao baada ya kubeba ubingwa mfululizo.

Watani wao wa wa jadi ni Curepipe Starlight SC ambao wanaona kama wamepokonywa umaarufu wa mji wa Curepipe na wapinzani wao hao, kamwe hawakubali kuwaunga mkono labda kundi dogo la wale wanaojiita ni wazalendo.

Curepipe Starlight angalau ni wakongwe na walianza kucheza mechi za kimataifa mapema. Mara ya kwanza ikiwa ni mwaka 2008 walipocheza Ligi ya Mabingwa Afrika, ikiwa ni baada ya kuwa mabingwa wa Mauritius mwaka 2007.
Uwanja wa Cercle de Joachim, maarufu kama Stade George V uliopo Curepipe katika wilaya maarufu ya Plaines unaingiza watu 6200 tu.

Bado soka ya Mauritius si kongwe na maarufu katika bara la Afrika. Soka lao si tishio sana na kwamba linaweza kuitikisa Yanga.

Lakini timu zao hazitabiriki kwa kuwa zina vijana wengi wenye vipaji na linachipukia kwa kasi kubwa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic