February 13, 2016



MPIRA UMEKWISHA
GOOOOOO Dk 90, Stand wanapata bao kupitia Osman ambaye anauwahi mpira mfupi uliikolewa na Nimubona na kuukwamisha wavuni
Dk 88, Maguri anashindwa kuuwahi mpira wa David Osman unatoka na kuwa goal kick

Dk 85, Stand wanaonekana kuchangamka zaidi huku Simba wakiwa kama wanarudi nyuma na wameridhika na mabao mawili, wanachofanya ni kulinda.

Dk 82, pasi safi anaipokea Kiiza, mara nyingine tena anageuka na kupiga vizuri kwa ufundi lakini mpira unapita juu ya lango.

Dk 74 hadi 79, Simba wanaumiliki zaidi mpira katika eneo la katikati ya uwanja. Stand wanaonekana kupoteana, hata hivyo hakuna mashambulizi makali kwenye upande wowote wa lango

Dk 72, Maguri anamlaghai Juuko na kupiga shuti kali, vile vile anashindwa kulenga lango
Dk 69, Chollo, beki wa zamani wa Simba anapiga shuti kali, almanusura, kama mpira ungeshuka kidogo, Simba wangezungumza mengine

Dk 66, Timu zinacheza zaidi katika ya uwanja, inaonekana wazi hakuna ufundi mwingine sana hasa katika kutafuta nafasi
Dk 51, Ajib anapiga shuti vizuri lakini kidogo hakuweza kulenga langoGOOOOOOO Dk 47, Kiiza anaifungia Simba bao la pili na kuonyesha ni mjanja hasa katika suala la kucheka na nyavu

Dk 46, Mechi imeanza na Simba wanaonekana kushambulia kwa kasi zaidi
MAPUMZIKO:
Dk 42 hadi 45, Mpira kidogo unaonekana kupoteza radha, hii inatokana na mvua inayoanza kunyesha na kusababisha wachezaji kupunguza ile kazi.

Dk 37, Kiiza anapoteza nafasi nyingine  zuri baada ya pasi nzuri ya Ndemla. Anashindwa kulenga lango
GOOOOOOO Dk 34, Simba inapata bao kupitia kwa Hamisi Kiiza ambaye sasa anaonakekana kuwa tishio sana.

Taratibu mashambulizi yanaanza, lakini Simba wanaonekana kuwa wazuri zaidi katika nafasi ya kiungo.


Mechi imeanza na timu zinaonekana kusomana na kucheza taratibu kama kila upande unahofia..

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic