February 3, 2016


Matope yanaonekana kuwapa wakati mgumu lakini Prisons ndiyo wanaofika mara nyingi kwenye lango la Yanga
DAKIKA TATU ZA NYONGEZA
Dk 87 Prisons wanapata kona, Asukile anaichonga vizuri lakini unapita na kuwa goal kick

GOOOOOOO Dk 85, Yanga wanafunga bao la pili baada ya shuti la Msuva kupanguliwa lakini linajaa wavuni
PENAAAAT Dk 84, Yanga wanapata penalti baada ya beki Prisons kuushika mpira kutokana na pasi ya chini ya Niyonzima
Dk Dk 76 hadi 81, Prisons wanapoteza muda zaidi kutokana na kuridhika na bao moja mbele ya Yanga
Dk 75,  krosi safi ya Niyonzima, Msuva anapiga kichwa lakini kipa anaokoa vizuri kabisa

Dk 67, Msuva peke yake eneo la hatari anashindwa kufunga na kupiga kichwa njeee
Dk 66, Niyonzima anapiga mkwaju wa faulo, unaokolewa na kuwa kona isiyokuwa na matunda
GOOOOOOOO Dk 62, Mohammed Mkopi anaruka na kufunga bao la pili kwa kichwa mbele Bossou

SUB Dk 53, Yanga inamtoa Boubacar nafasi yake anaingia  Simon Msuva
Dk 48, Yanga wanapata kona, Boubaccar anaichonga vizuri kabisa, lakini Prisons wanaokoa
Dk 47, krosi nzuri ya Niyonzima, kipa akiwa hayupo langoni, Ngoma anapiga kichwa lakini mabeki wanaokoa
Dk 46 mpira unaanza kwa Prisons kuwa wa kwanza kufika langoni mwa Yanga lakini Dida anakuwa makini

MAPUMZIKO
Dk 44, Chudu wa Prisons anagongana na Makapu, sasa anatibiwa
Dk 42, Twite anapiga shuti kali kabisa lakini unatoka sentimeta chache

GOOOOOOOOO Dk 40 Juma Jeremia Jeremiah Juma anaifungia Prisons bao safi kwa kichwa huku beki Bossou anabaki chini bila ya kuruka
Dk 39, Asukile anafanya kazi ya ziada na kuokoa mpira hatari wa krosi wa Joshua
GOOOOOOO Dk 35, Tambwe anaifungia Yanga bao safi kwa kichwa baada ya kuunganisha krosi nzuri ya Oscar Joshua
Dk 26 hadi 32, mpira zaidi unachezwa katikati ya uwanjani

Dk 25, kipa Prisons anafanya kazi ya ziada kuokoa mpira wa krosi wa Juma Abdul uliokuwa unaingia langoni na kuwa kona. Sasa anatibiwa
Dk 18 Yanga wanapata kona mbili mfululizo, lakini wanashindwa kuitumia
Dk 9, nusura mpira wa Bossou uingie langoni mwake, unatoka na kuwa kona.
Dk 4, Prisons  wanajaribu, shuti kali kabisa lakini Dida anawahi na kudaka
Dk 3, Twite anarusha mpira mrefu langoni mwa Prisons, lakini kichwa cha Tambwe, hakikulenga lango
Dk 1 Prisons wanaanza kufika kwenye lango la Yanga lakini mpira unaokolewa
YANGA:
1. Deo Munishi
2. Juma Abdul
3. Oscar Joshua
4. vicent Bosou
5. Mbuyu Twite
6. Said Juma ‘Makapu’
7. Deus Kaseke
8. Haruna Niyonzima
9. Donald Ngoma
10. Amissi Kiiza

11. Issouf Boubacar

1 COMMENTS:

  1. YANGA:
    1. Deo Munishi
    2. Juma Abdul
    3. Oscar Joshua
    4. vicent Bosou
    5. Mbuyu Twite
    6. Said Juma ‘Makapu’
    7. Deus Kaseke
    8. Haruna Niyonzima
    9. Donald Ngoma
    10. Amissi Kiiza

    11. Issouf Boubacar

    namba kumi ni sahihi mwandishi?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic