February 13, 2016


Na Mwandishi Wetu, Curepipe
Ijue Cercle de Joachim Sports Club, mabingwa wa Ligi ya Mauritian watakaochuana na Yanga, February 14 mwaka huu
Cercle de Joachim SC ni timu inayoshiriki Ligi Kuu ya Mauritius, makazi yake yakiwa katika jiji la Curepipe nchini humo.

Yanga inatua katika mji wa Curepipe kwa ajili ya mchezo wa leo wa Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa na uhakika wa kupata mashabiki kibao.

Mashabiki wa kikosi cha Curepipe Starlight watakuwa na kazi ya kuishangilia Yanga ambayo itacheza dhidi ya mahasimu wao wakubwa Cercle de Joachim kwenye Uwanja wa George V, mjini hapa.

Mechi hiyo inatarajiwa kuhudhuriwa na mashabiki wengi kutokana na sifa za ujio wa Yanga ambayo imekodi ndage kwa ajili ya mechi hiyo.

Cercle de Joachim ndiyo mabingwa mara mbili mfululizo wa Mauritius, jambo ambalo wapinzani wao hawataki kuliona.
Mashabiki wa Curepipe Starlight, furaha yao kubwa ni kuona wapinzani wao wanapoteza.

Hivyo watakuwa tayari kuiunga Yanga mkono kama ambavyo wamekuwa wakizungumza tokea mapema.

Mashabiki hao ambao wanaamini miaka miwili mfululizo imekuwa ya bahati kwa Cercle de Joachim, wanataka iishe na timu yao ianze kutamba.

Shangilia yao, huenda inaweza kuipa nguvu Yanga ili ijione ipo nyumbani na ipambane kwa nguvu zaidi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic