February 13, 2016

Kocha Selemani Matola amerejea Ligi Kuu Bara, safari hii akiwa ni kocha mkuu.

Matola amepanda amepanda baada ya kikosi chake cha Geita Gold Mine kushinda kwa mabao 8-0 dhidi ya JKT Kanembwa.

Ushindi huo umeifanya kufikisha pointi 30 sawa na Polisi Tabora lakini tofauti ya mabao ya kufunga imewabeba.


Polisi Tabora nayo imeitwanga JKT Oljoro kwa mabao 7-0, lakini haikuisaidia kuibuka na nafasi hiyo kutoka Kundi C.

Akizungumza kwa furaha kubwa, Matola amesema ni kitu ambacho alikipigania.

"Nina furaha sana, kwa kuwa nilikuwa nina ndoto hii. Nashukuru sana wachezaji, viongozi wa Geita Gold Mine pamoja na mashabiki wote," alisema Matola.

Polisi Tabora inabaki nafasi ya pili kwa kuwa imezidiwa mabao ya kufunga baada ya tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa kulingana.

Matola aliamua kuondoka Simba alipokuwa ni kocha msaidizi baada ya kuona hakuwa akipewa ushirikiano na kocha mkuu, Dylan Kerr raia wa Uingereza.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic