February 11, 2016


Simba imepanga kufanya mazoezi mara moja tu kwa leo katika maandalizi yake ya mwisho kabla ya kuwavaa Stand United, Jumamosi.

Simba iko mkoani Shinyanga ikijiandaa na mechi hiyo inayitarajia kupigwa kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.

Msemaji wa Simba, Haji Manara amesema Simba watafanya mazoezi leo mara moja na baada ya hapo, kesho itakuwa ni mapumziko.

“Hiyo ndiyo ratiba ya kocha, Ijumaa ni mapumziko. Naamini lengo litakuwa ni kupata mapumziko,” alisema.

Jana,Manara aliiambia SALEHJEMBE kwamba wamepata mapumziko ya kutosha wakiwa mjini Shinyanga, pia maandalizi ya kutosha huku akisistiza wanahofia mvua tu.


Simba iko katika nafasi ya pili ikiwa na pointi 42, huku vinara wa Ligi Kuu Bara kwa sasa Yanga wakiwa na pointi 43.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic