February 6, 2016


Februari 20, mwaka huu, Simba na Yanga zitacheza mechi ya raundi ya pili ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, lakini maneno ya kiungo wa Wekundu wa Msimbazi, Jonas Mkude si mazuri kwa wapinzani wao.

Mkude amesema, Yanga ikiwa na viungo wake Haruna Niyonzima, raia wa Rwanda na Thabani Kamusoko wa Zimbabwe, ijiandae kwa kipigo kwani kikosi chao kimeimarika sasa.

KAMUSOKO

Mayanja ameiongoza Simba katika mechi tano na kushinda zote, ambapo waliifunga Mtibwa Sugar bao 1-0, JKT Ruvu (2-0), Burkina Faso katika Kombe la FA (3-0), African Sports (4-0) halafu Mgambo JKT mabao 5-1. 

“Hivi sasa tupo vizuri, kazi yetu inaonekana uwanjani ambapo kila mchezaji ana morali ya hali ya juu, hivyo timu zote tutakazokutana nazo ikiwemo Yanga, zinatakiwa kujipanga, vinginevyo dozi itaongezeka.

MKUDE NA NIYONZIMA KAZINI....


“Tangu Mayanja alipochukua mikoba ya kuifundisha timu yetu, mechi yetu ya kwanza tulishinda bao moja, ya pili tukashinda mabao mawili, ya tatu tukashinda tatu, ya nne tukashinda nne na ya tano tukashinda tano, umeiona hatari hiyo kwa Yanga? Wajiandae,” alisema Mkude.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic