February 6, 2016




KRC Genk imeshinda kwa bao 1-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Ubelgiji huku mshambuliaji Mtanzania akianza rasmi leo safari yake ya kutimiza ndoto ya kucheza soka la kulipwa barani Ulaya.

Kwa mara ya kwanza, tena katika mechi ya Ligi Kuu Ubelgiji, Samatta ambaye ni mwanasoka bora Afrika ameichezea Genk kwa dakika 17.

Samatta aliingia katika dakika ya 73 katika mechi hiyo ya ugenini akichukua nafasi ya en Karelis.

Tayari wakati huo, Genk ilikuwa inaingoza kwa bao moja lililofungwa na Buffel katika dakika ya 62 na lilidumu hadi mwisho wa mchezo.

Kabla ya hapo, Samatta alipewa nafasi ya kufanya mazoezi na kikosi cha akiba, kabla ya kupelekwa katika kikosi cha kwanza ambacho leo amekichezea.

Samatta amejiunga na timu hiyo akitokea TP Mazembe ya DR Congo ambao ndiyo mabingwa wa Afrika.

VIKOSI:
Moeskroen : Vagner, Peyre, Castelletto, Dussenne, Mohamed, Hubert, Marquet (45' Markovic), Badri (56' Oussalah), Michel (69' Mulic), Coulibaly.

KRC Genk : Bizot, Walsh, Dewaest, Kabasele, Hamalainen, Ndidi, Kumordzi (58' Malinovsky), Buffel, Bailey, Kebano (83' Buyens) en Karelis (73' Samatta)
Doelpunten :

62' : 0 - 1 : Buffel

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic