February 13, 2016




Simba sasa ndiyo vinara wa Ligi kuu Tanzania Bara baada ya kufikisha pointi 44.

Hii ni mara ya kwanza Simba kukaa kileleni katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara.

Simba imeishinda Stand United kwa mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga, leo na kufanikiwa kufikisha pointi hizo. Shukurani kwa Hamisi Kiiza aliyepachika mabao yote mabili.

Huo ulikuwa ni mchezo wa 19 wa Simba ambayo inakaa kileleni dhidi ya Yanga wenye pointi 43 lakini wana michezo 18 kwa kuwa leo walikuwa na jukumu la michuano ya kimataifa.

Azam FC wanakuwa wa tatu na pointi 43, lakini wana viporo viwili na hawa ndiyo wenye nafasi kubwa ya kuing’oa Simba kileleni.

Hata hivyo, kama Simba itashinda mechi yake dhidi Yanga wikiendi ijayo, maana yake itakuwa ni mbio kali za kileleni kati ya Simba na Azam FC na kuiacha Yanga ikihangaika.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic