February 13, 2016

SINGANO (KUSHOTO) WKAATI AKIWA SIMBA AKIPAMBANA NA BOLOU WA AZAM FC.

Winga wa Azam FC, Ramadhan Singano ‘Messi’ amesema licha ya ushindani uliopo kamwe Simba na Yanga haziwezi kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara.

Messi aliyejiunga na Azam msimu huu akitokea Simba, amesema anaipa nafasi kubwa timu yake kutwaa ubingwa ligi msimu huu kwani wana kikosi kipana kinachoweza kupambana muda wote.

 Messi anaamini licha ya ushindani uliopo katika ligi, bado wanayo nafasi ya kuchukua taji hilo kwa mara ya pili.

“Ligi imebadilika hilo halina ubishi, ushindani umeongezeka kwa sababu mwanzo Yanga ndiyo walikuwa wana kasi pamoja na sisi lakini sasa Simba nao wamekuja juu na kila mmoja anautaka ubingwa.


“Lakini nadhani kwa upande wetu bado tunayo nafasi ya kuchukua ubingwa licha ya ushindani huo maana timu yetu ina kikosi kipana cha ushindani tofauti na wapinzani wetu,” alisema Messi.

SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic