February 13, 2016

PINTO


Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (Taswa), kimeshtushwa na kitendo cha kiungo wa Simba, Mwinyi Kazimoto kumpiga mwandishi wa michezo wa Kampuni ya Mwananchi Communication Limited, Mwanahiba Richard.

Katika taarifa yake iliyotolewa jana na Mwenyekiti Juma Pinto, Taswa imezungumza na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, ACP Mika Nyange na Rais wa Simba, Evans Aveva ili kufahamu hali ya upelelezi ilipofikia ili haki ipatikane haraka. 

“Tumeweza kuzungumza na upande wa pili, kwa viongozi wa Simba kujua kama nao wao wamebaini kosa la mchezaji wao na Aveva ameahidi kutoa ushirikiano,” alisema Pinto. 


Pinto alisema Taswa inalaani tukio hilo. Katikati ya wiki hii, Kazimoto alituhumiwa kumshambulia Mwanahiba kwenye Uwanja wa Kambarage muda mfupi baada ya mazoezi ya timu yake kwa madai ya kumuandika vibaya siku za nyuma.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic