March 15, 2016


Na Saleh Ally
Kuchanganya siasa katika mambo ya soka au michezo kwa ujumla yamekuwa kati ya mambo yanayokwamisha kabisa maendeleo.

Inawezekana kabisa sehemu maendeleo yakapatikana bila kuwepo siasa. Katika michezo si lazima siasa ili maendeleo yapatikane.

Lakini barani Afrika, michezo na hasa wa soka umekuwa ukikwamishwa na siasa.

Wako wanautumia mchezo huo ili kufanikiwa na maisha yao nje ya soka, hasa wanasiasa. Pia wengine wenye tamaa ya maendeleo ya maisha yao binafsi.

Wakati Kenya walipompata Mwenyekiti kijana kabisa wa Shirikisho la Soka Kenya (FKF), Nick Mwendwa, kulikuwa na sifa nyingi kwamba enzi za kina Sam Nyamweya zimepita.

Naungana na wanaoona sasa ni wakati wa vijana kwamba kasi inayohitajika ni ile ya nguvu sana ili kuendana na mbiombio za maendeleo kisoka dunia.


Lakini nilipona picha ya Mwendwa ikisambazwa mitandaoni, ikimuonyesha akiwa amekaa sehemu ya kawaida, viatu vyake vikisafishwa, nikaona ni yaleyale.

Pamoja na kwamba sijawahi kukutana na Mwendwa, lakini kwa kuwa BLOG hii inasomwa sana Kenya, nimeona nimpe salamu zangu.

Mazingira ya picha hilo yanaonyesha kuna mazingira ya kujionyesha. Kutaka kuonyesha ni mtu wa watu, tena anaonekana alijua anapigwa picha.


Kama ilitumika wakati wa kampeni, sawa, lakini lazima akumbuke kuachana na siasa hizo kwa kuwa kaingia madarakani na watu wanataka mafanikio si hadithi.

Lakini kama ilipigwa baada ya uchaguzi, basi ni kosa kubwa sana na lazima Mwendwa akubali alichokifanya ni kupoteza muda na wapenda soka wa Kenya wanachotaka ni maendeleo kwa vitendo kupitia mafanikio.

Si kumuona ni mtu wa watu au aliye karibu na watu wengi. Hiyo itakuwa ni kupoteza muda kabisa.


Kenya nayo inayumba, ligi bado si imara sana, hakuna njia imara ya kukuza watoto na vijana, bado kuna migogoro rundo na wengi wanaiba tu katika mirija ya mchezo wa soka. Apambane na hayo ili kuibadili Kenya na kupitia mhimili wake kuwa na mabadiliko na maendeleo. Kila la kheri.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic