March 16, 2016


MPIRA UMEKWISHAAAA
GOOOOOOOO  Dk 88 Arsenal wanafanya kosa tena, Messi mbele ya beki Gabriel anamiliki mpira vizuri uliomtoka Neymar na kuuiinua unampita juu kipa Ospina na kuandika bao la tatu kwa Barcelona, maana yake Barcelona wana 5 na Arsenal moja
KADI Dk 84, Giroud analambwa kadi ya njano kwa kuudunda mpira kwa jazba baada ya kuambiwa amemfanyia madhambi Alba
Dk 79, Kipa Stegen wa Barcelona anafanya kazi ya ziada kuokoa mpira wa adhabu ndoto wa Sanchez, pia anaokoa shuti la Giroud. lilikuwa shambulizi zuri kwa Arsenal

KADI Dk 78, Turan analambwa kadi ya njano kwa kucheza faulo
Dk 77, hadi sasa kila timu imepata kona sita, Arsenal imepiga mashuti 10 nje ya lango, Barcelona imepiga 4

SUB Dk 75 Arda Tutan anaingia kuchukua nafasi ya Rakitic kwa upande wa Barcelona
Dk 74, Barcelona wanagongeana vizuri sana, lakini shuti la Raktic linapaaaaaa
SUB Dk 72, Arsenal inamuingiza Walcott kuchukua nafasi ya Danny Welbeck na Iwobi anatoka anaingia Olviere Giroud

SUB Dk 71 inamuigiza kiungo Sergio Reberto kuchukua nafasi ya Iniesta
Dk 70, Arsenal imemiliki mpira kwa 38% Na Barcelona kwa 62%
Dk 66, nafasi nyingine nzuri kwa Arsenal lakini shuti la Iwobi linagonga mwamba na kutoka nje

GOOOOO Dk 65, Suarez anaifungia Barcelona bao la pili baada ya krosi safi kutoka kulia iliyochongwa na Dani Alves
Dk 61, Arsenal wanacheza vizuri, Sanchez anapiga shuti Bosquet anaokoa inakuwa kona. Inachongwa na kumkuta Welbeck, anapiga kichwa safi kabisa

DK 60, pasi nzuri ya Rakitic, inamkuta Messi anajaribu shuti lakini linatoka nje mbali kabisa
Dk 57, Welbeck anapoteza nafasi nzuri kwa Arsenal, alibaki dhidi ya Mascherano akapata nafasi ya kupiga lakini bado beki huyo akaweka mguu na kuwa kona isiyo na mashara

Dk 55, Barcelona wanaingia vizuri kabisa na Messi anapiga shuti kali lakini Ospina anaonyesha uimara wake kwa mara nyingine
GOOOOOOO Dk 50, Arsenal wanapata bao safi kabisa kupitia Mohamed Elneny
KADI Dk 49, Sanchez analambwa kadi ya njano kwa kumuangusha Neymar

Dk 48, Iwobi anajaribu, anapiga shuti lakini Barcelona wanaokoa na kuwa kona
Dk 46, Barcelona ndiyo wanaonekana kuanza mashambulizi kwa kasi zaidi
MAPUMZIKO
Dk 45, Suarez anapoteza nafasi nyingine kwa kupiga shuti nyanya baada ya Messi na Iniesta kugongeana vizuri kabisa
SUB Dk 44 Arsenal inamtoa Flamini anaingia Coquelin, inaonekana ni kuhofia kadi ya njano aliyopata kwamba anaweza kupata nyekundu

Dk 42, Arsenal wanaonekana kucheza vizuri lakini makosa yanakuwa kwenye pasi za mwisho wanapoingia kwenye eneo la hatari la Barcelona

Dk 39, Arsenal wanapoteza nafasi nyingine baada ya kichwa alichopiga Sanchez, mpira unapita nje kidogo ya lango...
Dk 37 na 38, Arsenal wanashambulia mfululizo na wanapoteza nafasi mbili moja kupitia Iwobi

Dk 34 tayari Barcelona imepiga mashuti matatu yaliyolenga lango na Arsenal haijapiga hata moja
Dk 33, Barcelona wanapata kona nyingine ambayo inachongwa na Neymar, haina madhara
UMILIKI Dk 32 Hadi sasa Barcelona imemiliki mpira kwa asilimia 67 na Arsenal 33%

KADI Dk 31, Flamini analambwa kadi ya njano kwa kumfanyia faulo Iniesta
Dk 29, shuti safi la Neymar baada ya kupokea pasi ya Alba, lakini Ospina anadaka vizuri kabisa
Dk 29, Arsenal wameamua kurudi wote kila wanaposhambuliwa na wanatoka watatu haraka mbele wanapoanza kushambulia
Dk 27, Alba anaingia vizuri na kupiga krosi, inazuiliwa na Flamini kuwa kona, lakini haina matunda. Kona tena kutoka kwa Suarez 
Dk 26, Tayari Barcelona wamepiga mechi 111 zilizofika na Arsenal wamepiga 79
Dk 25, Arsenal wanapata kona, shuti safi kabisa la Flamini lakini linapita juu kidogo ya lango la Barcelona

Barcelona haijapoteza mechi ya pili baada ya kushinda ya kwanza katika Ligi ya Mabingwa Ulaya tokea walipofungwa na Metz mwaka 1984.

Kila upande unaonekana kuwa makini, Arsenal wanacheza vizuri tatizo linaonekana umaliziaji au mipango ya mwisho wanapkuwa langoni mwa Barcelona
GOOOO Dk 18 Neymar anaipatia Barcelona bao baada ya pasi nzuri ya Suarez

Dk 15, Messi anapata pasi nzuri ya Neymar lakini kipa Ospina anafanya kazi ya ziada kuokoa na kuwa kona
Dk 11, Arsenal wanapoteza nafasi baada ya Ozil kupiga shuti safi lakini hakulenga

Mechi imeanza na inaonekana kama kuna uoga kwa kila sehemu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic