March 16, 2016

MTAKA
Mwenyekiti wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Anthony Mtaka, amefanikiwa kuula baada ya kuteuliwa na Rais wa Tanzania, John Magufuli kuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu akiwa miongoni mwa wakuu wa mikoa 26 wapya walioteuliwa hivi karibuni.

Mtaka amesema kuwa amefurahia kuona amepewa nafasi hiyo ya kuwemo kwenye serikali ya awamu hii ambapo atahakikisha anatumia madaraka yake kuweza kuhakikisha mchezo wa riadha unapiga hatua.

“Ni jambo zuri na nimelipokea vyema, kuona nimekuwa sehemu ya serikali hii ya Magufuli baada ya kuchaguliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu ambapo nitahakikisha ninafanya vyema kwenye nafasi hii pamoja na kuusaidia mchezo wa riadha kwenda mbele zaidi ya hapa ulipo,” alisema Mtaka.


SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic