March 16, 2016


Makamu wa Rais wa Simba, Geofrey Nyange ‘Kaburu’, amesema kocha wa kikosi chao, Jackson Mayanja, amejitahidi kwa kiasi kikubwa kubadili mambo hata kuliko ilivyokuwa kwa makocha Wazungu waliopita Simba.

Kaburu ameiambia SALEHJEMBE kuwa Mayanja amebadili mambo mengi katika saikolojia kwa wachezaji, lakini hali ya utimilifu wa mwili, hivyo ni jambo jema kumuacha aendelee na anachokifanya huku uongozi ukibaki nyuma yake na kumuunga mkono.

“Hakika amejitahidi sana, angalia timu inavyocheza kwa kupambana kwa dakika zote 90. Timu ina nguvu na kasi, hakika wanacheza vizuri.

“Kama unakumbuka, Simba tulikuwa tunapambana kipindi cha kwanza na kufanya vizuri. Tukiingia kipindi cha pili mabao yote yanarudi.

“Kama uongozi tunamuunga mkono kocha na wachezaji wote kwa asilimia mia na moja. Tunamuacha aendelee kuongoza kikosi chake huku akipata sapoti yetu.

“Kama uongozi, hatuwezi kukaa tu kimya, badala yake kwenye ushauri tutashauri na tutashirikiana na wote. Hongera kwake, pia kwa wachezaji,” alisema Kaburu.

“Kazi ya Mayanja ni kuzidi hata ya makocha Wazungu. Wachezaji kuipatia klabu ubingwa ni wajibu wao. Uongozi pia tutakuwa karibu yao ili waendelee kupambana.”

Simba kwa sasa iko kileleni mwa Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 54 ikiwa inafuatiwa na Yanga yenye pointi 50 na Azam FC pointi 47.

Wakati Simba imecheza mechi 23, Yanga imecheza mechi 21 na Azam FC imecheza 20. Timu hizo zinategemea viporo vyake ili kuikamata Simba.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic