March 27, 2016



Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) leo limetangaza viingilio vya mchezo wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa Afrika (AFCON) kundi G siku ya Jumatatu kati ya Tanzania dhidi ya Chad, bei ya chini ikiwa ni shilingi elfu tano (5,000) tu.

Viingilio vya mchezo huo vimegawanyika katika makundi matatu, ambapo kiingilio cha juu kitakua shilingi elfu ishirini na tano (25,000) kwa VIP A, na shilingi elfu ishirini (20,000) kwa VIP B, na kwa viti vya rangi ya bluu, kijani na orange itakua shiligi elfu tano (5,000).

Tiketi za mchezo huo zitaanza kuuzwa kesho Jumapili saa 2 asubuhi katika vituo vinne ambavyo ni kituo cha mafuta Buguruni (Buguruni), Ubungo Oilcom (Ubungo) na Dar Live (Mbagala), na Jumatatu tiketi zitauzwa katika viunga vya uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Wakati huo huo Rais wa TFF, Jamal Malinzi amemshukuru Waziri Mkuu wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Majaliwa Kassim Majaliwa kwa kubali kuwa mgeni rasmi katika mchezo kati ya Tanzania v Chad utakaochezwa siku ya Jumatatu jijini Dar es salaam.

TFF pia inamshukuru Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye kwa kufanikisha ujio wa Waziri Mkuu kwa kufuatilia kwa karibu maombi ya TFF ya tarehe 21/03/2016 ya kumuomba Waziri Mkuu awe mgeni rasmi katika mchezo huo.

Kwa upande wa Taifa Stars iliyoweka kambi katika hoteli ya Urban Rose inaendelea na mazoezi katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, kujiandaa na mchezo wa marudiano dhidi ya Chad.


Waamuzi wa mchezo huo kutoka nchini Djibouti wanatarajiwa kuwaisli leo jioni ambao ni mwamuzi wa kati Djamel Aden Abdi, Abdilahi Mahamoud, Farhan Bogoreh Salim, Farah Aden Ali, huku kamisaa wa mchezo akiwa Andrea Abdallah Dimbiti kutoka nchini Sudani Kusini.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic