March 21, 2016

KANFIR

Kocha Mkuu wa APR ya Rwanda, Nizar Khanfir, raia wa Tunisia, amewatoa hofu wapenzi na mashabiki wa Yanga kwa kusema kwa jinsi Yanga inavyocheza, ana imani itavuka hatua inayofuata na kufika mbali zaidi kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Yanga imeingia hatua ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya juzi Jumamosi kuiondoa APR kwa jumla ya mabao 3-2 na sasa itakutana na Al Ahly ya Misri huku mchezo wa kwanza ukitarajiwa kupigwa jijini Dar mapema mwezi ujao na kurudiwa baada ya wiki mbili huko Misri.

Al Ahly nayo baada ya kulazimisha suluhu ugenini katika mchezo wa awali, juzi Jumamosi iliichapa Recreativo do Libolo ya Angola mabao 2-0 na kuifuata Yanga ambayo misimu miwili iliyopita, timu hizo zilikutana kwenye michuano hiyohiyo na Yanga kutupwa nje kwa mikwaju ya penalti baada ya matokeo ya jumla kuwa 1-1.

Khanfir amesema Yanga imekuwa ikibadilika kulingana na timu inayokutana nayo, hivyo kuna uwezekano mkubwa wa kufika mbali zaidi ya ilipo sasa ikichagizwa na kuwa na wachezaji wengi wazoefu.

“Mchezo kwa jumla ulikuwa mzuri kwa pande zote, tulipata nafasi tukafunga na wao wakapata wakafunga, lakini kila timu ilikuwa na uwezo wa kusonga mbele kwa jinsi mchezo ulivyokuwa wa wazi na kama tungepata bao lingine, naamini hali ingebadilika na lolote lingetokea.


“Tayari tumetolewa na naipongeza Yanga kwa kupita na kuingia hatua inayofuata, ni matumaini yangu kuwa Yanga itafika mbali zaidi kutokana na kucheza kwao kwa kujitambua, wana wachezaji wazoefu, pia wanabadilika kulingana na wakati, hivyo hatua waliyoingia wanaweza kuvuka,” alisema Khanfir.

1 COMMENTS:

  1. Tunaamini wanabebwa,lakini kwa hayo uliyosema mmmmh!hapo inabidi tufumbe midomo yetu.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic