March 26, 2016


Kocha wa Simba, Jackson Mayanja amesema atasimamia nidhamu ndani ya kikosi chake muda wote na mchezaji atakayeenda kinyume atamtimua hata kama ni muhimu kikosini.

Mayanja alisema bila nidhamu timu haiwezi kupata mafanikio hivyo kwake yeyote atakayeenda kinyume atamtimua hata Hamis Kiiza anayeongoza kwa ufungaji kwenye Ligi Kuu Bara akiwa na mabao 19.

Kauli hiyo ya Mayanja raia wa Uganda imekuja siku chache baada ya kumtimua beki Abdi Banda aliyegoma kupasha misuli moto wakati Simba ikicheza na Coastal Union hivi karibuni kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Pia Mayanja aliwahi kumsimamisha beki wa kati Hassan Isihaka aliyehoji kuhusu kuwekwa benchi mbele ya wenzake.  

Mayanja alisema amejipanga vilivyo kuhakikisha anaimarisha nidhamu ndani ya Simba kwa faida ya timu na siyo kwa ajili yake.

“Mchezaji yeyote atakayekwenda kinyume na hilo hatapona hata kama ni Kiiza. Katika hili kusema kweli sitoangalia mtu au uwezo wake wa kucheza soka nachotaka mimi ni mchezaji kuwa na nidhamu.

“Hata akiwa Kiiza, Juuko Murshid au Brian Majwega ambapo tunatoka wote Uganda wakionyesha utovu wa nidhamu nitawachukulia hatua.

“Sipendi kabisa mchezaji awe juu ya timu ila nataka mchezaji awe chini ya timu, hata kama kuna watu watapiga kelele juu yangu katika hilo, hakika sitajali kwani ninachotaka ni kuiona Simba inafanya vizuri,” alisema Mayanja.


Katika hatua nyingine, Manyanja alisema amefurahishwa kumuona beki wake wa kati, Isihaka kwenye kikosi cha timu hiyo baada ya kumaliza kuitumikia adhabu yake ya kusimamishwa mwezi mmoja.

Source: Championi

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic