March 18, 2016



Beki wa pembeni wa Azam FC, Shomari Kapombe, amefunguka kuwa licha ya kufanikiwa kufunga bao lake la nane katika mchezo wa juzi Jumatano dhidi ya Stand United, bado analikumbuka  bao alilofunga katika mchezo dhidi ya Yanga  ambalo lilikataliwa.

Katika mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam, Kapombe alifanikiwa kufunga bao pekee na kufikisha mabao nane sawa na John Bocco, mshambuliaji wa Azam FC ambaye amewahi kuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara.

Kapombe alisema kuwa sababu kubwa inayomfanya aendelee kufunga mabao mengi ni kutokana na kitendo chake cha kucheza kwa kujituma ili kuhakikisha wanafanikiwa kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu Bara licha ya kuachwa na Simba kwa tofauti ya pointi nne.

“Nadhani suala kubwa lililopo ambalo limekuwa likinisaidia katika kufanya vizuri ni kumuomba Mungu na kujituma hakuna kitu kingine zaidi ya hicho kwa sababu ushindani umekuwa mkubwa kila timu inahitaji ipate matokeo sasa lazima tupambane ili kufikia malengo.


“Unajua kwa sasa kufunga kwangu nadhani ni kitu muhimu katika kila mchezo ili niweze kufanikisha hilo japokuwa bao nililofunga katika mchezo dhidi ya Yanga lilikataliwa sijui kwa nini, maana huenda sasa yangefikia tisa,” alisema Kapombe.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic