March 28, 2016

JAMAL MALINZI, RAIS WA TFF

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limeshtushwa na matokeo ya mchezo wa kupata bingwa wa Mkoa wa Katavi baada ya timu ya Stand FC kuibuka na ushindi wa mabao 16-0 dhidi ya Kamazima hali ambayo TFF imekiagiza Chama cha Soka Mkoa wa Katavi (KRFA) kufanya uchunguzi wa matokeo hayo.

Mchezo huo uliopigwa juzi Jumamosi, ulikuwa ni wa kumpata bingwa atakayeuwakilisha mkoa huo kwenye Ligi ya Mabingwa Mkoa ambayo inatarajiwa kuanza hivi karibuni.

Kabla ya mchezo huo wa mwisho, timu ya Nyundo FC ilikuwa inaongoza kwa kuwa na pointi 21 na mabao 24 ya kufunga, ambapo Stand FC ilikuwa ikihitaji ushindi wa mabao 13-0 ili kuweza kuwa bingwa wa mkoa huo.

Taarifa iliyotumwa jana na TFF, imesema: “Baada ya Stand kushinda kwa mabao 16-0, inaonyesha kuna dalili za upangaji wa matokeo, hivyo KRFA haitaruhusiwa kutangaza bingwa wa mkoa huo hadi uchunguzi utakapokamilika na TFF ijiridhishe na uchunguzi huo.”

Ikumbukwe kuwa, hivi karibuni TFF ilizuia kuitangaza timu iliyopanda daraja kutoka Kundi C la Ligi Daraja la Kwanza kutokana na kuhisi kuwepo kwa vitendo kama hivyo ambapo katika mechi za mwisho, Geita Gold Sport iliifunga JKT Kanembwa mabao 8-0, huku Polisi Tabora ikiinyuka JKT Oljoro mabao 7-0.


2 COMMENTS:

  1. Goli 8-0 na 7-0 katika mchezo wa soka mbona ni matokeo ya kawaida?Mbona yanga ilifungwa 5-0 na Simba hamkufanya uchunguzi kama yanga ilihongwa?Kwa hiyo TFF haitaki timu yenye uwezo ishinde kwa magoli ya kutosha?Huo ni ujinga uliopitiliza,Stars ilipigwa 7 na Algeria,mbona TFF haikuiomba CAF/FIFA iichunguze Stars kama ilihongwa na Algeria?Au kwa kuwa TFF ndiyo inayoisimamia Stars,yenyewe ndiyo iliyohongwa na Algeria ndiyo maana haikulalamika?

    ReplyDelete
  2. Anonymous goli 7'8'9 sio ishu sana tatizo ni goli 16 kiakili hata we ukifikiri utaona kunaupangaji wa matokeo. Kama walikuwa na uwezo hebu tupe score zao zote toka mechi ya kwanza mpa hiyo ya mwisho uone kama wana ushindi wa zaidi.ya goli 4. Sio lazima kucomment sometime usoma tu na kupita na zako.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic