March 23, 2016


Saa chache baada ya Simba kuwasilisha barua yake kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye ikilalamikia viporo vya Yanga na Azam FC, Bodi ya Ligi (TPLB) kwa kushirikiana na TFF zimetangaza kufanya mabadiliko.

Mabadiliko hayo yanaonyesha Yanga na Azam FC zitacheza viporo vyake haraka na ndani ya siku 11, zitalazimika kucheza mechi tatu wakati Simba itacheza mechi moja tu.

Yanga na Azam FC zitalazimika kucheza mechi kuanzia Aprili 3, Aprili 6 na Aprili 13 wakati huo Simba itacheza mechi moja tu ya Aprili 11. Maana yake sasa timu hizo zitakuwa zimecheza mechi sawa kwa kuwa sasa zina mechi 2 zaidi ya Simba. 

Ndani ya kipindi hicho cha siku 11, Azam FC na Yanga watacheza mechi tatu na Simba itacheza mechi moja.

Aprili 3, Yanga itakuwa Dar es Salaam kuivaa Kagera Sugar na Azam FC itakuwa ugenini CCM Kirumba jijini Mwanza kuivaa Toto African.

Aprili 6; Yanga itarejea dimbani Taifa kuivaa Mtibwa Sugar na Azam FC itakuwa Chamazi ikikaribisha Ndanda FC ya Mtwara.

Aprili 11, Simba nayo itashuka Uwanja wa  Majimaji mjini Songea kuwa wageni wa Majimaji, kwa maana hiyo, Yanga na Azam FC bado zitakuwa na mechi moja kiporo tena.


Aprili 13, Yanga na Azam FC zitashuka “kubalance”, Yanga itacheza Mwadui FC kwenye Uwanja wa Taifa na Azam FC itacheza dhidi ya Mtibwa Sugar ikiwa ugenini Manungu, Turiani.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic