March 14, 2016



Jopo la madaktari raia wa India, wamekabidhiwa beki wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ kusimamia majeraha yake ya kifundo cha mguu ‘enka’.

Hiyo yote ni katika kuhakikisha anapata matibabu mazuri na haraka ili arejee uwanjani kuisaidia timu hiyo inayoshiriki Ligi ya Mabingwa Afrika, Kombe la FA na Ligi Kuu Bara.

Awali, beki huyo alikuwa akipatiwa matibabu hayo ya enka kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kabla ya kuhamishiwa Hospitali ya London Health Centre ya jijini Dar es Salaam inayohusika na masuala ya mifupa.

Cannavaro alisema baada ya kugundulika hana tatizo kubwa la kusababisha afanyiwe upasuaji, jopo hilo la madaktari limemuandalia kliniki maalumu chini ya madaktari raia wa India.

Cannavaro alisema kliniki hiyo  atakayoihudhuria itaenda sambamba na matibabu, pia programu maalum ya mazoezi kwa ajili ya kuimarisha mifupa yake.

Aliongeza kuwa, kliniki hiyo ataihudhuria hospitalini hapo kwa muda wa wiki tatu kabla ya wiki inafuata kuanza mazoezi ya pamoja na wenzake.

“Katika kupunguza gharama za kwenda kwenye matibabu nchini India, uongozi wa Yanga umenihamishia kwenye hospitali maalumu inayohusiana na matibabu ya mifupa pekee ambayo ipo hapa nchini.

“Hospitalini hapo, huduma inayotolewa ni ya mifupa ambayo tayari nimeanza matibabu yangu ya enka iliyoniweka nje ya uwanja tangu Novemba.


“Ninahudhuria kliniki kila baada ya siku tano huku nikifanyishwa mazoezi maalum na madaktari hao, hiyo yote ni katika kuhakikisha ninapona na ninarejea uwanjani haraka kuitumikia timu yangu ya Yanga,” alisema Cannavaro.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic