March 19, 2016



Kikosi cha Armee Patriotique Rwandaise (APR) leo Jumamosi jioni kinacheza na Yanga mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, wenyeji wanatakiwa kujichunga na mambo yafuatayo.

APR itapanga wachezaji 11 uwanjani kwa mujibu wa kanuni, kati yao wapo watano ambao ni hatari na bila ulinzi wa kutosha kwao lolote laweza kutokea.

Kocha msaidizi wa APR inayomilikiwa na Jeshi la Rwanda, Willson Byuse anasubiri Yanga iteleze tu ili wapate ushindi na kusonga mbele akimsaidia kocha mpya, Nizar Khanfir raia wa Tunisia.

Wa kwanza anayepaswa kuchungwa ni kiungo mkabaji, Yannick Mukunzi anayevaa jezi namba sita, beki Emery Bayisenge (jezi namba tano) na winga Sibomana Patrick , huyu anavaa jezi namba 11.

Mwingine ni nahodha Jean Claude Iranzi anayevaa jezi namba 12 na kiungo mchezeshaji, Djihad Bizimana, huyu huvaa jezi namba nane pia ni mjomba wa Haruna Niyonzima.

Muunganiko wa wachezaji hao ni hatari na hata Kocha Byuse amesema kuwa; “Yanga wakijisahau kidogo tu wameumia kama wao walivyotufunga nyumbani tulipojisahau.”


Ili isonge mbele, APR inatakiwa kupata ushindi wa mabao 2-0, au wowote unaofanana na huo kwani nyumbani kwao walifungwa mabao 2-1.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic