April 3, 2016



Azam FC imetoka sare ya bao 1-1 dhidi ya wenyeji wake Toto African kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, leo.

Sare hiyo inaifanya Azam FC kuangusha pointi mbili kutokana na sare hiyo mjini Mwanza. Hiyo ni nafuu kubwa kwa Simba.

Azam FC ilikuwa inafukuzia pointi 9 katika mechi zake tatu za kiporo, lakini sare hiyo inaifanya iwe imedondosha pointi mbili baada ya sare hiyo kwenye uwanja uliojaa maji na tope.

Sare inaifanya Azam FC kuwa na pointi 51, inaendelea kubaki katika nafasi ya tatu na Yanga inakuwa katika nafasi ya pili baada ya kushinda leo bao 3-1 dhidi ya Kagera Sugar, sasa ina pointi 53.

Simba iko kileleni ikiwa na pointi 57 lakini imecheza mechi mbili zaidi ya Yanga na Azam FC ambazo kila moja ina mechi 22 na Simba imecheza 24.


Kama Azam FC itashinda mechi zake mbili zijazo, ndiyo itakuwa na pointi 57, sawa na Simaba na kama itapata sare nyingine, maana yake haitaweza kuifikia Simba.

1 COMMENTS:

  1. Bado wana nafasi kwani lazima mechi za nyumbani washinde,
    na bado lazima simba akalishwe na azam na kupoteza point 3.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic