April 13, 2016


Azam FC imekula vizuri kiporo chake kwa kuichapa Mtibwa Sugar kwa bao 1-0.

Licha ya Mtibwa Sugar kuwa nyumbani Manungu, Turiani lakinilishindwa kuizuia Azam FC iliyopata bao pekee kupitia kwa nahodha wake John Bocco katika dakika ya 61 kupitia mkwaju wa penalti.

Pamoja na ushindi huo, Azam ilipata pengo kwa kiungo wake Himid Mao kulambwa kadi nyekundu baada ya kuanzisha mzozo na watu wa huduma ya kwanza.

Ushindi wa leo unaofanya Azam FC kufikisha pointi 55 baada ya kucheza mechi 24 Simba akiendelea kuwa kileleni.

Tayari Azam imekamilisha viporo vyake baada ya mchezo wa leo na imekuwa katika nafasi nzuri baada ya kuibuka na ushindi.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic