April 9, 2016



Acha na klabu zenyewe kuneemeka, Azam FC na Yanga zikifuzu kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho basi Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) litapata fedha kutokana ushiriki wa timu hizo.

Yanga ipo katika Ligi ya Mabingwa Afrika, lakini ikitolewa na Al Ahly itakwenda kwenye Kombe la Shirikisho ambako inaweza kufuzu hatua ya makundi sawa na Azam ambayo tayari ipo katika michuano hiyo.

Azam yenyewe inatakiwa kwanza kuitoa Esperance ya Tunisia katika hatua ya 16 Bora, halafu icheze tena mtoano na timu kutoka Ligi ya Mabingwa Afrika ndipo ifuzu hatua ya makundi.
Kuna uwezekano mkubwa Azam na Yanga ama kukutana katika makundi Kombe la Shirikisho au zenyewe kucheza mtoano kuwania kufuzu hatua hiyo.

Kama zote zikifuzu hatua za makundi basi kila timu haikosi dola 150,000 sawa na Sh milioni 321 ambayo ni zawadi ya Shirikisho la Soka Afrika (Caf) kwa timu inayoshika mkia miongoni mwa timu nne.

Utaratibu wa Caf ni kutoa fedha pia kwa shirikisho au chama cha soka ambako timu inatokea, hivyo kwa anayeshika nafasi ya nne chama chake cha soka kitapata dola 15,000 sawa na Sh milioni 32.

Ikiwa Azam na Yanga zikifuzu, TFF itapata Sh milioni 64, timu ikishika nafasi ya tatu itapata dola 239,000 sawa na Sh milioni 511, hapo TFF itapata dola 20,000 sawa na Sh milioni 42. Kucheza nusu fainali ni sawa na aliyeshika nafasi ya tatu.

Bingwa atapata dola 625,000 sawa na Sh bilioni 1.3 na TFF hapo itapata dola 35,000 sawa na Sh milioni 74. Mshindi wa pili atapata dola 432,000 sawa na Sh milioni 924 na TFF itapata dola 30,000 sawa na Sh milioni 64.


1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic