April 27, 2016


Kiungo mkongwe wa zamani wa Yanga, Athumani Idd ‘Chuji’, mwishoni mwa msimu huu amepanga kuondoka kwenye timu yake ya sasa ya Mwadui FC inayofundishwa na Jamhuri Kihwelo ‘Julio’.

Mkongwe huyo ni mmoja wa wachezaji waliofanya kazi kubwa ya kuipandisha daraja timu hiyo hadi Ligi Kuu Bara msimu huu kwa mara ya kwanza baada ya kumaliza mkataba wa kuichezea Yanga.

Kiungo huyo hivi sasa ni mchezaji huru kutokana na kubakiza mwezi mmoja kwenye mkataba wake unaomalizika mwishoni mwa msimu huu pamoja na mshambuliaji wa timu hiyo, Jerry Tegete.

Chuji amesema ni ngumu kuwepo kwenye timu isiyokuwa na imani na yeye, hivyo ameona ni bora akaenda kwenye timu yenye imani naye.

Chuji alisema kwenye mechi mbili muhimu mfululizo, zote amewekwa benchi dhidi ya Yanga kwenye ligi kuu na nusu fainali ya Kombe la FA dhidi ya Azam FC bila kupewa sababu huku akipata taarifa za chini kwamba uongozi hauna imani naye huenda akaihujumu timu, kitu ambacho siyo sahihi.

“Mimi maisha yangu nayaendesha kwa kucheza soka na kikubwa ninataka kuonekana, sasa kocha anaponiweka benchi kwenye mechi muhimu anakuwa ananiharibia na ninashindwa kuonekana.

“Kwa mfano, mechi dhidi ya Yanga na Azam zote niliwekwa benchi nikiwa nipo fiti kabisa, lakini cha ajabu wachezaji kwenye timu wananifuata wakilalamika kwa nini sichezi wakati ni mchezaji muhimu.


“Nakosa jibu la kuwapa na mara zote huwa nakaa kimya tu, nimeona ni bora nikaondoka Mwadui na kwenda kutafuta maisha kwingine nitakapopata nafasi ya kucheza na nashukuru zipo baadhi za timu zinanifuatilia,” alisema Chuji. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic