April 29, 2016


Azam TV wataionyesha moja kwa moja mechi kati ya Azam FC dhidi ya Simba. Mechi inayosubiriwa kwa hamu kuu.

Mechi hiyo ya Ligi Kuu Bara ni muhimu zaidi na maradufu kwa Simba. Kwa kuwa kama itapoteza mechi hiyo, itakuwa imejiondoa rasmi katika mbio za ubingwa.

Simba ina pointi 57 katika nafasi ya tatu, Azam FC ina 58 katika nafasi ya pili. Simba inahitaji kushinda ili kuendelea kuwa katika mbio hizo.


Kama itaishinda Azam FC itakuwa imefikisha pointi 60 na kupanda hadi nafasi ya pili. Kwa kuwa Yanga ndiyo vinara na tayari wana pointi 62 kabla ya kuivaa Toto African kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, kesho. 

2 COMMENTS:

  1. waandishi wa siku hizi bwana, story kibao lakini unasahau taarifa muhimu kabisa, hio mechi inachezwa lini? unadhani wasomaji wako wate wana ratiba ya TFF?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ndiyo wandishi wetu hao. Ushabiki mbele.

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic