April 18, 2016

Mshambuliaji wa Leicester City, Jamie Vardy yupo kikaangoni na anaweza kuongezewa adhabu ya kufungiwa kutokana na kuonyesha utovu wa nidhamu katika mechi ya jana dhidi ya West Ham United.

Vardy alipewa kadi nyekundu katika dakika ya 56 ikiwa ni njano ya pili kutokana na kuonekana amejiangusha katika eneo la 18, katika mchezo huo uliomalizika kwa sare ya mabao 2-2.



Baada ya kupewa kadi hiyo na mwamuzi Jon Moss, straika huyo ambaye ni Mwingereza alionyesha kuwa na hasira na kuanza kumsonta Moss huku akizuiliwa na wenzake kabla ya kuondoka uwanjani hapo.

Vardy atakosa mchezo mmoja kutokana na kadi hiyo nyekundu ambapo atakosa mchezo ujao dhidi ya Swansea City, Jumapili ijayo, lakini kama FA ya England itapitia tukio hilo anaweza kukosa mechi nyingine ijayo dhidi ya Manchester United, Mei mwaka huu.

Hivi karibuni straika wa Chelsea, Diego Costa aliadhibiwa kukosa mechi moja na faini ya pauni 20,000 na kupewa onyo kali kutokana na kuonyeaha utovu wa nidhamu kwa mwamuzi Michael Oliver baada ya kupewa kadi nyekundu katika mechi dhidi ya Everton.

Alipoulizwa juu ya tabia ya mchezaji wake na kama ataongezwa adhabu, Kocha wa Leicester, Claudio Ranieri alisema: Sitaki kuzungumza suala la mwamuzi na Vardy. Nyie (waandishi) mliona tukio hilo vizuri zaidi yangu, nataka niwe mpole nizungumze kuhusu masuala ya soka."

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic