April 27, 2016


Makamu wa Rais wa Simba, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ leo anatarajiwa kuiongoza Kamati ya Mashindano ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kujadili mchezo wa Kombe la FA hatua ya nusu fainali uliozikutanisha Yanga na Coastal Union.

Mchezo huo uliopigwa wikiendi iliyopita kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, ulivunjika dakika ya 105 baada ya kutokea vurugu zilizosababisha mwamuzi, Abdallah Kambuzi kuuvunja mchezo huo. Mpaka mchezo huo unavunjika, Yanga ilikuwa ikiongoza kwa mabao 2-1.

Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya TFF, Jemedari Said, alisema kikao hicho kitajadili mechi zote mbili za nusu fainali ili kubaini kama kulitendeka haki au la.

“Kamati itakayokaa itakuwa ikiongozwa na mwenyekiti, Geofrey Nyange ‘Kaburu’, na hii itakuwa ikijadili mechi zote hizo mbili na siyo ya Yanga pekee, huwezi jua katika mchezo wa Azam dhidi ya Mwadui kuna tukio gani lilitokea.

“Huu umekuwa utaratibu wa kila baada ya mechi lazima tukae kujadili matukio, najua watu wengi wanataka kufahamu hatima ya mchezo kati ya Yanga na Coastal, lakini nje ya uwanja huwezi jua kama kuna timu ilifanya tukio gani,” alisema Said.

Mbali na Kaburu kuwa mwenyekiti wa kamati hiyo itakayokaa leo, makamu mwenyekiti ni Said Mohammed, katibu, Jemedari Said huku wajumbe wakiwa ni Ahmed Mgoi, James Mhagama, Stuart Masima, Philip Njowoka, Clement Sanga (makamu mwenyekiti Yanga) na Boniface Wambura.


Ikumbukwe kuwa, mchezo wa Azam na Mwadui, uliisha kwa Azam kushinda kwa penalti 5-3 baada ya kumaliza dakika 120 wakiwa sare ya mabao 2-2. 


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic