April 8, 2016


Azam FC imepata pigo la kuuguliwa na beki wake wa kulia, Shomari Kapombe ambaye amelazimika kusafirishwa kwa ajili ya kufanyiwa matibabu ya haraka nchini Afrika Kusini.

Kapombe ambaye amefunga mabao nane katika Ligi Kuu Bara, amekosa mechi mbili zilizopita kutokana na kusumbuliwa na tatizo la homa ya mapafu ikielezwa kuwa lilianza kumsumbua katika mechi dhidi ya Prisons ambayo alishindwa kucheza dakika 90.

Kapombe aliyetarajiwa kuondoka jana saa saba mchana kuelekea Johannesburg, atapata matibabu kwa siku mbili kisha kurejea nchini.

Kocha Mkuu wa Azam, Stewart Hall, amesema: “Kapombe bado ana umri mdogo, anastahili matibabu ya uhakika zaidi pia tunataka arejee mapema uwanjani, ndiyo maana kumekuwa na safari hiyo ya matibabu.”


Kwenye listi ya wafungaji wa Azam msimu huu katika ligi kuu, Kapombe anashika namba tatu akiwa nyuma ya washambuliaji John Bocco mwenye mabao tisa na Kipre Tchetche aliyefunga mabao 10. 

SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic