April 4, 2016


SIKU MBEYA CITY ILIPOINGIA MKATABA NA BIN SLUM, HAPA ILIWAKILISHWA NA MMOJA WA WAKURUGENZI WAKE, MOHAMMED BIN SLUM (KULIA).

Mdhamini wa Mbeya City, Nassor Bin Slum amesema anatarajia kuongeza mkataba mwingine wa miaka miwili ya kuidhamini timu hiyo iwapo itabakia ligi kuu msimu ujao.

Mbeya City, ambayo ilikuja kwa kasi wakati ilipopanda ligi kuu msimu wa 2013/14 na kumaliza ikiwa nafasi ya tatu ya msimamo wa iliingia udhamini na Bin Slum kwa muda wa miaka miwili ambao unatarajia kufikia tamati mwishoni mwa msimu huu.

NASSOR BIN SLUM
Hata hivyo, timu hiyo ipo nafasi ya 12 ya msimamo kwa sasa ikiwa na pointi 24 nyuma ya Kagera Sugar yenye pointi 25 na iwapo itafanya vibaya katika mechi zake zilizobakia itakuwa kwenye hatari ya kushuka daraja.

 Bin Slum amesema kuwa, timu hiyo haifanyi vizuri lakini ameridhika na jinsi inavyomtangaza ikiwa ni pamoja na kuheshimu mkataba walioingia na kudai kuwa ataongeza mkataba mwingine wa miaka miwili iwapo timu hiyo itabaki ligi kuu msimu ujao na ikishuka ndiyo anaagana nayo.

“Timu haifanyi vizuri, lakini naridhika na kwa jinsi wanavyonitangaza vyema katika kila mechi wanayocheza, ni watu wanaoheshimu mkataba, Mbeya City wanajitahidi, nitaongeza mkataba mwingine nikimaliza huu na nimewapa masharti, wamesema watajipanga ili kurudisha makali yao ya msimu uliopita.

“Kasi waliyoionyesha msimu huu ni tofauti na msimu uliopita, lakini kwa sasa nipo katika mazungumzo ya kuongeza mkataba mwingine wa miaka miwili ijayo.


“Mkataba wa safari hii nitakaoingia nao utakuwa ni wa masharti tofauti na ilivyokuwa hapo nyuma na iwapo watashuka daraja basi itakuwa ndio mwisho umefikia kwani moja ya masharti yangu ni kudhamini timu ambazo zipo ligi kuu tu,” alisema Bin Slum.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic