April 19, 2016

KIUNGO wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, Jean Mugiraneza ‘Migi’, amesema kuwa licha ya timu hiyo kukabiliwa na mchezo mgumu wa ugenini dhidi ya Esperance, bado ina nafasi ya kusonga mbele kwa kuwatoa waarabu hao na kutinga hatua ya 16 bora ya Kombe la Shirikisho Afrika.
KIKOSI CHA AZAM FC

Azam FC tayari imewasili nchini Tunisia kwa ajili ya mchezo huo wa marudiano utakaofanyika leo Jumanne saa 3.00 kwa saa za Afrika Mashariki, wameingia wakiwa na kumbukumbu ya ushindi wa mabao 2-1 walioupata awali jijini Dar es Salaam.

Migi amesema Azam FC ina wachezaji wengi wazoefu na wazuri jambo ambalo linampa matumaini ya kufanya vizuri katika mchezo huo.

“Nawajua Esperance, nimecheza nao mara nne nilipokuwa nacheza APR, mara zote nyumbani kwetu tulikuwa tunatoa nao sare au kushinda bao moja, lakini wamekuwa wakitufunga kwao, wanapocheza nyumbani wanapenda sana kumiliki mpira kwa kucheza pasi na pia waamuzi mara nyingi walikuwa upande wao kuwapendelea,” alisema.
 Migi alisema wanatakiwa kuwa makini sana katika mchezo huo kwa kukabiliana na presha kutoka kwa wapinzani wao ili waweze kupata matokeo wanayohitaji.

Kiungo huyo kutoka Rwanda tangu ajiunge na Azam FC, Julai mwaka jana, amekuwa nguzo muhimu kwa timu hiyo kwenye eneo la kiungo wa ukabaji, akiwa na uwezo wa kucheza mipira ya juu na ya chini pamoja na kutibua mashambulizi ya timu pinzani.

Azam FC inahitaji sare yoyote au ushindi ili iweze kusonga mbele kwa hatua ya 16 bora (play off), itakapokutana na moja ya timu iliyotoka kwenye hatua hiyo ndani ya Ligi ya Mabingwa Afrika na ikifuzu hapo itatinga moja kwa moja katika hatua ya makundi ya michuano hiyo (robo fainali).

SOURCE: AZAMFC.CO.TZ

KIKOSI CHA ESPERANCE

WACHEZAJI WA AZAM WAKIFANYA MAZOEZI KUJIANDA NA MECHI YA PILI DHIDI YA ESPERANCE.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic