April 11, 2016

EVOUNA
Straika wa Al Ahly, Malick Evouna, ameshangazwa na jinsi Yanga walivyocheza kwenye mchezo wao wa juzi Jumamosi wa Ligi ya Mabingwa Afrika na kusema kuwa mchezo wao wa marudiano utakuwa mgumu.

Yanga na Al Ahly zilikutana Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar, kwenye mchezo wa raundi ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika uliomalizika kwa sare ya 1-1 na zinatarajiwa kurudiana kati ya Aprili 19 na 20.

Mshambuliaji huyo ambaye alicheza mechi hiyo kwa dakika tano akiingia akitokea benchi kuchukua nafasi ya Moamen Zakaria, amesema kuwa kwa muda wote aliokuwa benchi alikuwa akiusoma mchezo huku akishangazwa na Yanga walivyokuwa wakicheza kwa kuonyesha upinzani, tofauti na alivyotarajia. 

Alisema kuwa Yanga wana uwezo mkubwa wa kusonga mbele lakini amebaini kitu kitakachowaangusha ni kutojiamini kwao.

“Mchezo ulikuwa mzuri kwa upande wetu lakini pia nawapongeza Yanga kwa jinsi walivyocheza, wametupa upinzani tofauti na tulivyotarajia.

“Uwezo wa kusonga mbele wanao, hatutawadharau hata kidogo kwenye mchezo ujao, kuna kitu ambacho kinawaangusha, nilipokuwa benchi nilikuwa nawaona wanacheza bila kujiamini, kama watajiamini wanaweza kutufunga,” alisema Evouna.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic