April 25, 2016


Na Saleh Ally
HAKUNA kitu Watanzania wengi hawakipendi kama ukweli. Ukikisimamia, basi wewe ndiye adui namna moja wa wengi, lakini mimi naendelea tu na leo nipo Tanga.

Kwanza nianze kulaani kitendo cha mashabiki waliokua kwenye Uwanja wa Mkwakwani wakati Coastal Union ikipambana na Yanga katika nusu fainali ya Kombe la FA kumpiga mwamuzi msaidizi hadi akazimia.

Hakika ameumizwa na mara nyingi nimekuwa nikilalama kuhusiana na vurugu za uwanja huo, hadi imefikia sipendi hata kuangalia mpira hapo.

Ingawa safari hii, unaweza ukasema ni kama nyuki waliochokozwa, si kama siku nyingine. Mwamuzi msaidizi aliyekuwa ameshika kibendera upande wa mashariki ya uwanja. Alifanya mambo mawili makubwa na mabaya katika mpira wa nchi hii.

Hakuna anayeweza kukataa hata kidogo kama Coastal Union waliutawala hasa mchezo huo. Walikuwa bora mara mbili ya Yanga, wachezaji vijana na wazalendo walikuwa bora mara tatu zaidi ya wakongwe na wageni wanaolipwa mamilioni ya fedha ukilinganisha na wao.

Coastal Union wenyewe wanapaswa kujilaumu kushindwa “kuua” mchezo mapema kabisa. Walikuwa na uwezo wa kwenda mapumziko na bao tatu na Yanga, walikubali kabisa. Lakini hawakuwa makini na mambo yakawa magumu kabisa.


Bao la Coastal Union lililofungwa na Yossouf Sabo raia wa Cameroon lilikuwa bora na bomba kweli. Lakini mabao yote mawili ya Yanga yalijaa utata na lile la pili linaonyesha ni uonevu wa dhati, dhahiri shahiri kwamba mwamuzi huyo alipanga kuona Yanga inashinda. Huu ni upuuzi wa hali ya juu ambao tunataka tukae kimya na kuuachia upite kwa kuwa kila mmoja anahofia kulaumiwa na mashabiki wa Yanga kama atasema ukweli.

Yanga ilikuwa na mabao 2-1 hadi mwamuzi anavunja mchezo baada ya vurugu. Lakini uhalisia unaonyesha “hapana”. Bao la kwanza alilofunga Donald Ngoma, lina utata mkubwa wa kuotea, Ngoma anafunga lakini hata yeye anaonyesha hajiamini kama anapaswa kushangilia au la.

Bao la pili la Tambwe, dhahiri anausukuma mpira kwa mkono kila mmoja akiona wazi. Lakini mwamuzi anaamua kusema bao. Hakika hii ni aibu na Wanayanga wanaochukia watu kusema ukweli watakuwa ni wanaojidanganya kwa kuwa bingwa wa michuano hiyo atashiriki michuano ya kimataifa ambako hakuwezi kuwa na waamuzi wazembe kama hao wa mechi kati ya Yanga dhidi ya Coastal Union.


Mwisho wa hili. Adhabu inaweza kuangukia kwa Coastal Union na Yanga ikasonga ikionekana haina hatia. Lakini macho yetu yanapeleka ujumbe ndani ya mioyo yetu kwamba Coastal Union wameonewa au wamedhulumiwa.

Dhuluma hiyo unaweza kuikataa kinafiki, lakini kama ni muungwana. Kamwe hauwezi kuwaza hilo, badala yake utakasirishwa kabisa hata kama utakuwa Yanga wa kulialia.
Lazima kuwe na “fea” game. Kama Coastal waliitoa Simba, mwamuzi akatoa penalti dakika ya mwisho kwa kuwa yalikuwa ni maamuzi sahihi, hicho ndicho kinachotakiwa kwa kuwa tunahitaji bingwa halali.

Angalia mechi ya Mwadui FC dhidi ya Azam FC ilivyokuwa tamu. Angalia ushindani wa juu na mshindi mwisho kapatikana kwa mikwaju ya penalti.


Mechi ya Tanga; gumzo lake sasa ni uamuzi mbovu. Hakika hili ni jambo baya katika soka nchini kwetu na haitakuwa ni kuisaidia Yanga, pia uzembe wa mwamuzi huyo hauwezi kuwa na faida katika mchezo wa soka na TFF wanapaswa kuchukua hatua kali pamoja na maumivu ya kipigo alichopata, lakini apumzishwe kabisa.

Sitaki hata kukumbuka kilichotokea, naona aibu. Jana usiku, nimejitahidi nikilala nisiote ndoto ya mechi hiyo, naogopa!



19 COMMENTS:

  1. Unajitahidi kuonesha uko upande gani halafu unajiita mwandishi wa michezo. Hivi kama mwamuzi alikuwa anampango wa kuibebe yanga kwa nini asilikatae goli la Coastal, kama mwamuzi alikuwa na mpango wa kuibeba Yanga kwa nini alikataa goli la kamusoko. Kama kumiliki mpira ndio kushinda ina maana Yanga kule Misri ilishinda? na je mbona Barcelona walifungwa na Real tena wakiwa pungufu. kama ishu ni goli la mkono mbona maradona aliwafunga waingereza lakini mwamuzi hakupigwa lakini zaidi ya yote tujiulize Coastal walikuwa wapi siku zote hizo mpaka sasa wako katika hatari ya kushushwa daraja kwenye ligi? Kumbukumbu zinaonyesha hii si mara ya kwanza kwa washabiki wa Coastal kufanya vurugu msimu huu na misimu iliyopita mkajipange

    ReplyDelete
    Replies
    1. Huyu mwandishi sijui kasomea wapi taaluma yake. Ana kawaida ya kuandika hisia zake na kuzifanya ndiyo halisi

      Delete
  2. Punguza unazi wewe.

    Siku za nyuma ulituhakikishia kuwa Aden Rage kala hela za uhamisho wa Okwi. Matokeo yake? Uongo wako umeonekana dhahiri baada ya Simba kulipwa fedha zake japo zimecheklewa.

    Siku zote ndiyo aina ya uandishi wako.

    ReplyDelete
  3. COASTAL KWA TABIA YAO CHAFU NI BORA WASHUKE DARAJA.
    NI WATU WA FUJO,HAWAFAI,BORA WAMEKUTANA NA KIBOKO YANGA,MAANA TUKILALAMIKA SISIS WENGINE TUKAONEKANA WAONGO NA KWAMBA TUMEZOEA KUONGEA HASA TUNAPOKUWA TUMESHINDWA.

    ReplyDelete
  4. It was really not fair line two did wrong

    ReplyDelete
  5. Una tatizo la mapenzi. Hufai kua mwandishi kwa kua bias. Woga wako yanga watakutana na mwajili wako azam. COast km ni wzr wasingekua wanapigana kubaki ligi kuu. ooh ngoma kaotea sasa ulitaka mwenye makosa ngoma au refa? Goli la mkono toka jana we peke ako unaongea hbr iyo as if ulikua uwanjan peke ako. Punguza mapenz y uwanasimba hata yanga warudiane na cost mwisho wa cku tutakutana na bi mdogo ako azam.

    ReplyDelete
  6. Siku nyingi nilishatoa tahadhari kwa TFF kuwachukulia hatua baadhi ya makocha akiwemo Julio waliokuwa wakitoa kauli za kuwabeza waamuzi kwamba wanachochea washabiki na ipo siku yatakuja tokea maafa.Watanzania lazima tukubali kwamba katika mpira mtaalamu wa kanuni 17 za soka ni refa na ndio mwenye kauli ya mwisho uwanjani,kama ilivyo kwa Hakimu ayu Jaji mahakamani na Daktari hospitalini,awe amekosea au hakukosea kauli yake ni ya mwisho na ambaye hakubaliani naye anatakiwa kwenda ngazi inayofuata sio kulalamika pembeni au kufanya fujo.Kama Coastal wangekuwa wazuri wangefunga magoli halafu refa ayakatae sana sana tunaona Yanga ndio waliofunga goli refa akakataa.Wastanzania tubadilike ulaya kila siku yanafungwa magoli yenye utata lakini hatuoni washabiki wakifanya fujo bali makocha kutimuliwa

    ReplyDelete
  7. we saleh acha uongo .leo ndio unajua maonevu. umesahau ulikua unamsia costa alivyokua analeta vurugu mechi dhidi ya arsenal .na kwa uonevu refa badala ya kumtoa costa .akaishia kuwapa redcard arsenal. na katika makala zako zilivyo bomuuu. ukamsifia sana costa .ukasema ame win game jwa chelsea .sasa leo inakuaje unamlaumu mshika kibendera na mwamuzi. wakati yanga wame win game tena bila ya kumpiga mtu.au macho yako
    siku nyingine hua una yakalia yanaona unacho taka wewe. ni hii blog yako mbovuuuuu.kwanza coastal hawana lolote mpira ni timming tu .yanga wametoka safari wamechoka
    na wamefanya kila kitu ku win game km costa alivyofanya. na dk zilikua bado nyingi kwa nini coastal km ni timu nzuri wasitumie kupata ushindi. au pia haujawahi kuona ikiongoza na kupoteza mchezo mwisho. ndio maana wanaume hua wanapambana mpaka dk ya mwisho.

    ReplyDelete
  8. Mpumbavu tu huyu mbna la kurusha mawe ambalo hata kwa wanaojua Mpira ndo kosa la kulaani kwanza anakomaa na muamuz huu.uchambuz mavi wajue hiz link zinahitaji wasomi na sio unazi

    ReplyDelete
  9. Tatizo shule tangu lini mchambuzi hajawahi hata kucheza mpira wa ushindani???

    ReplyDelete
  10. Dah yaani saleh ally kaniboa nilikuwa napenda sana kusoma champion na blog yake ya saleh jembe from kesho sotoingia tena ktk blog yake na wala sitonunua tena champion kwani kwani sitokubali kuwa mfuasi wa makala zake zenye unazi wa wazi kwake....hate you bro

    ReplyDelete
  11. Dah yaani saleh ally kaniboa nilikuwa napenda sana kusoma champion na blog yake ya saleh jembe from kesho sotoingia tena ktk blog yake na wala sitonunua tena champion kwani kwani sitokubali kuwa mfuasi wa makala zake zenye unazi wa wazi kwake....hate you bro

    ReplyDelete
  12. napenda kuwajibu yanga wote mnaodai habari imeandikwa kiushabiki. hivi huyu saleh ni mshabiki wa timu ngapi? ameshaandika ukweli kuhusu simba je alikua mshabiki wa yanga? alishaandika ukweli kuhusu azam je alikua mshabiki wa simba? tatizo lenu yanga hamtaki ukweli ila mmekuta saleh jembe hayupo katika list ya wanaopokea vibahasha vya yanga kila mwezi kama akina mbole mbole na dick dauda. maana kule ndio sehemu pekee ambapo kila siku kuna makala zaidi ya moja kuiponda simba na zaidi ya tatu kuisifia yanga. mlibebwa na mtaendelea kubebwa chini ya tff ya jamal malinzi hilo Halina ubishi ila ngoma inakua ngumu mkienda helua helua. saleh kila siku anapost muro anavyoiponda simba mnafurahi, saleh alimuhoji davis mosha mnafurahi ila akisema nyie ni tandale modern taarab wana mbeleko imekua nongwa. naamini kabisa saleh ni miongooni mwa waandishi wachache wa habari za michezo wasionunulika bongo ndio maana habari zake haziegemei upande mmoja ila zinasimama ktk ukweli. usirudi nyuma jembe japo mimi naamini waandishi wa habari za michezo bongo wana mchango mkubwa ktk kuua soka letu lkn nna imani na wewe.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Huyu siku zote anaandika kiushabiki. Iwe ni kuhusu Yanga au Simba. Inaelekea anaokota maneno ya vijiweni na kuyaandika kama kweli tupu. Rejea suala la malipo ya Okwi. Ilikuwa rahisi kudhani Aden Rage alikula hela hizo kumbe ilikuwa uongo mtupu. Bila shaka alipata maneno hayo kwenye vijiwe vya wapinzani wa Rage. Amwombe radhi Rage.

      Delete
  13. Wachambuzi wa bongo hao huwa hawafichi hisia zao shaffih dauda Saleh jembe ni wanazi wakubwa wa msimbazi

    ReplyDelete


  14. ;-) pole bro ulichoandika kinajijibu chin

    ReplyDelete
  15. Salehe ushindwe na ulegee kwa Jina la Yesu..

    ReplyDelete
  16. Toka lini mtu akaotea kwa kukimbiwa angalia vizur utaona ngoma anapokea mpila akiwa hajaotea beki wa kati anakimbia kutoka nyuma kwenda mbele muwe makini na mkiandikacho

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic