April 6, 2016


KIIZA...
Uongozi wa Klabu ya Simba umesema straika wao, Hamisi Kiiza na beki wa timu hiyo, Juuko Murshid, watatakiwa kuandika barua za kujieleza kutokana na kuchelewa kujiunga na wenzao ambao wapo katika maandalizi ya michezo ya Ligi Kuu Bara na Kombe la FA.

Tangu wachezaji hao raia wa Uganda waondoke nchini wiki mbili zilizopita kwenda kuitumikia timu yao ya taifa katika michezo ya kufuzu Michuano ya Mataifa Afrika (Afcon 2017) dhidi ya Burkinafaso, mpaka leo bado hawajarejea huku kukiwa hakuna taarifa zozote zinazoeleza juu ya kuchelewa kwao.

Ofisa Habari wa Simba, amesema uongozi wa klabu hiyo umepanga kuwandikia barua ya kujieleza na kutolea ufafanuzi wa kile kilichowafanya kuchelewa kurudi kujiunga na wenzao.

JUUKO
Wachezaji hao wamezidisha siku sita tangu siku ambayo walitakiwa kurejea kuungana na wenzao.

Katika hatua nyingine, Manara alisema sakata la beki wao, Abdi Banda limepelekwa katika Kamati ya Nidhamu ya Simba na huko ndipo watatoa hukumu ya kesi yake.


Banda kwa sasa amesimamishwa na Simba kwa kile kilichoelezwa ni kumgomea kocha wake, Jackson Mayanja alipomtaka aingie uwanjani kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Coastal Union uliopigwa Machi 19, mwaka huu katika Uwanja wa Mkwakwani, Tanga na Simba kuibuka na ushindi wa mabao 2-0.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic