April 27, 2016



AmissiTambwe amesema amefunga bao halali dhidi ya Coastal Union na anawashangaa wanaodai kafunga kwa mkono wakiwemo mashabiki na maofisa wa Simba, timu aliyoichezea kabla ya kujiunga na Yanga.

Tambwe aliifungia Yanga bao la pili dakika ya 104, katika muda wa nyongeza katika mchezo wa nusu fainali ya Kombe la FA dhidi ya Coastal Union Jumapili iliyopita kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Bao hilo lilizua tafrani kiasi cha mashabiki wanaodaiwa kuwa wa Coastal Union kurusha mawe uwanjani na mwamuzi Abdallah Kambuzi kuvunja mchezo huo huku mwamuzi msaidizi Charles Simon akipigwa na jiwe usoni. 

Wakati mchezo huo ukivunjika, Yanga ilikuwa mbele kwa mabao 2-1 na hatma yake itafahamika leo Jumatano kutoka Kamati ya Mashindano ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
Baadhi ya mashabiki wa soka nchini wakiwemo wa Simba na hata Ofisa Habari wa timu hiyo, Haji Manara, walinukuliwa wakisema bao alilofunga Tambwe halikuwa sahihi kwani alifunga kwa mkono.

Tambwe amesema, alifunga bao hilo kwa kifua na siyo mikono kama inavyodaiwa.

“Najua ni kwa nini bao hilo limewauma sana Simba, wengi wao walitaka kuiona Yanga nayo inatolewa katika michuano hiyo kama ilivyokuwa kwao, ndiyo maana wameumia sana.

“Nawaomba Simba wakae kimya kwani bao langu haliwahusu kama walikuwa wanadhani Yanga tutatolewa hatua ya nusu fainali basi imekula kwao waache maneno ya kichochezi,” alisema Tambwe.


Kama Yanga ikipelekwa katika fainali ya Kombe la FA, itacheza na Azam FC ambayo iliifunga Mwadui FC kwa penalti 5-3 baada ya sare ya mabao 2-2 kwenye Uwanja wa Mwadui Complex mkoani Shinyanga wikiendi iliyopita.

SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic