April 22, 2016

MANARA
BAADA ya hivi karibuni beki wa kulia wa Simba, Hassan Kessy kutamka kuwa hataweza kuendelea kuitumikia klabu hiyo baada ya mkataba wake kumalizika, uongozi wa timu hiyo umemjibu kuwa hauwezi kumzuia mchezaji huyo kama ataamua kuchukua maamuzi hayo.

Kessy amesimamishwa kuitumikia klabu hiyo kwa michezo mitano ya Ligi Kuu Bara iliyosalia huku akiweka wazi kuwa hawezi kuongeza mkataba kuitumikia timu hiyo.

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Simba, Haji Manara, ameliambia Championi Ijumaa kuwa, Kessy ameikuta Simba na hata akiondoka wao wataendelea kuwepo.

“Tunajua kuwa mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu huu, ni uamuzi wake abaki au la, lakini hata kama akiamua kuondoka, hatuwezi kumzuia kutokana na hayo kuwa ni maamuzi yake binafsi. Ameikuta timu kwani ilikuwepo kabla yake.

“Ajue kwamba Simba siyo ya baba yake wala ya mama yake, kama kaamua hivyo aende tu maana nimekuwa nikimtetea tangu alipofanya makosa kwenye mechi dhidi ya Yanga, hizi ni klabu za umma na sisi viongozi tunatukanwa sana kila tunapofungwa. 

KESSY
“Kama hataki maneno kama hayo anayoambiwa basi akacheze bao, aache kujihusisha na soka na kama ameamua kucheza soka basi mambo hayo ni ya kawaida tu,” alisema Manara.




0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic